- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DC MTATIRO AFANYA KIKAO KAZI NA MAAFISA TARAFA NA WATENDAJI WA KATA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro leo tarehe 3 April, 2024 amefanya kikao kazi na Maafisa Tarafa wa Manispaa ya shinyanga na wa Halmashauri ya Wilaya ya
shinyanga pamoja na watendaji wa kata kutoka Manispaa ya shinyanga na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika ukumbi wa lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika kikao hiki Mhe. Mtatiro amewapongeza kwa ufanyaji kazi mzuri katika majukumu yao huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwahudumia wananchi vizuri pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati.
“ Niwapongeze kwa utendaji kazi wenu mzuri katika majukumu yenu ya kila siku, lakini endeleeni kufanya kazi kwa bidii kwa kuwahudumia wananchi vizuri pamoja na kusikiliza kero zao na kuzitatua kwa wakati”. amesema Mhe. Mtatiro
Aidha, Mhe. Mtatiro amewataka Watendaji hao kufikia tarehe 15 April, 2024 kila sehemu inayotoa huduma kwa wananchi ikiwemo , vituo vya afya, Zahanati, Hospital, Mashuleni na Masokoni kuhakikisha wanabandika namba yake ili wananchi wanapohitaji kufanya mawasiliano wakati wowote wanapopatwa na changamoto na kupata msaada wa haraka.
Pamoja na mambo mengi Mhe. Mtatiro amewaagiza Maafisa Tarafa na Watendaji wa kata kwenda kufanya mikutano na watumishi wao wa chini , kufanya mikutano ya hadhara kwa wananchi ya kusikiliza kero na kutatua kero mbalimbali kila mwezi, kwenda kufanya uhamasishaji katika swala la lishe mashuleni, uhamasishaji wa upandaji miti ya kutosha katika Taasisi mbalimbali, Kaya pamoja na kwenda kusimamia miradi ya maendeleo yenye kuendana na thamani ya fedha zinazotolewa na serikali .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutenga muda na kuwakumbusha majukumu mbalimbali Watendaji hao na kuahidi kwenda kusimamia maagizo yote aliyoyatoa
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga