- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katiba Tawala wa wilaya ya shinyanga Ndg. Said Kitinga ameongoza kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe kwa robo ya nne (Aprili-Juni 2022/2023) kwa niaba ya Mhe. Johari Samizi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Lewis kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga kilijumuisha viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya shinyanga na Manispaa ya Shinyanga akiwemo Afisa lishe wa Mkoa Ndg Yusuph Hamis.
Ndg. Said ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho pamoja na mambo mengine amewataka wajumbe wote kushirikiana kwa pamoja katika kufanya siku ya afya na lishe katika kata zote na kufanya ajenda hii ya lishe iwe ya kudumu katika vikao na mikutano.
"Niwatake wajumbe wote tushirikiane kwa pamoja katika kutekeleza swala zima la lishe kwa kufanya siku ya Afya na lishe katika kata zote lakini pia ajenda hii ya lishe iwe ya kudumu katika vikao na mikutano yetu tunayoifanya ikiwa ni katika kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ambae anakipa kipaumbele suala la lishe bora nchini " alisema Ndg. Said
Kwa upande wake Afisa lishe Mkoa Ndg. Yusuph Hamis amewataka Watendaji wa kata kusimamia kwa ukaribu wanafunzi wote waweze kupata chakula mashuleni ili kuzidi kuongeza ufaulu zaidi.
Ikumbukwe uwepo wa lishe bora Nchini itasaidia wananchi kuwa na afya nzuri na kuwawezesha kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi mapana kwa Taifa zima kwa ujumla.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga