- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
DAS KITINGA AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA PEPMIS MANISPAA YA SHINYANGA
Na. Shinyanga Mc
Katibu Tawala wa wilaya Ndg. Said Kitinga leo tarehe 5 Novemba amefungua mafumo wa usimamizi wa utendaji kazi kwa watumishi wa Umma kwa njia ya kieletroniki (PEPMIS) katika ukumbi wa kalinjuna uliopo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo washiriki wa mafuzo haya ni walimu wakuu wa shule pamoja na waratibu elimu kata.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo haya Ndg. Kitinga amewataka washiriki wa mafunzo wawe wasikivu ili waweze kupata uelewa wa pamoja kwani baada ya mafunzo haya hawatatumia mfumo wa zamani (Oprass) na badala yake wataanza kutumia mfumo wa (PEPMIS) .
"Muwe wasikivu na mpate uelewa wa pamoja kwani baada ya mafunzo haya hatutatumia tena mfumo wa zamani badala yake tutatumia mfumo mpya wa kieletroniki wa (PEPMIS) hivyo lazima kila mmoja ashiriki mafunzo haya" amesema Ndg. Kitinga
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Bi. Getruda Gisema amewasihi washiriki wafuatilia kila hatua ambayo wanafundishwa kwani kila hatua inategemeana na nyengine kwa kuwa mfumo huu ni muhimu na niwa lazima kila mtumishi wa serikali atautumia katika kupimwa utendaji kazi wake.
Mfumo wa PEPMIS utasaidia watumishi wa Umma kufanya majukumu yao kwa weledi pia kupitia mfumo huu utasaidia kufanya tathmini ya rasimali watu katika halmashauri ili kujaza ziada na upungufu uliopo katika maeneo mbalimbali kwa kuangalia muda na utaalamu walionao watumishi wa umma.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga