- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika kuhakikisha afya bora ya mifugo na kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya homa ya mapafu kwa ng’ombe na ugonjwa wa Sotoka kwa mbuzi na kondoo Chanjo itakayotolewa itakayotolewa kwa siku 10 ndani ya Halmashaurii
Wakizungumzia juu ya Ujio wa Chanjo hiyo ya Ruzuku Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga wameishukuru serikali kwa kuwaletea Chanjo hiyo Inayolenga kuboresha Afya za Mifugo yao na kuongeza tija Katika zao la Mifugo Hali inayowawezesha kujipatia kipato kutokana na ushindani wa Mifugo zao la Mifugo.
Ndg.Jumapili Robert ni Afisa Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Shinyanga amesema bei halisia ya Chanjo hiyo ni Tsh 1000 kwa kila Ng'ombe ambapo kutokana na mpango wa Ruzuku Mfugaji atachangia Tsh. 500 na 300 kwa Mbuzi badala ya Tsh 600 kama bei halisia ya Chanjo kwa Mbuzi.
Mkuu wa Idara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Manispaa ya Shinyanga Ndg. Revocatus Lutunda akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwal. Alexius Kagunze Mwitikiowa wafugaji ni Mzuri wafugaji
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Neema Rwegoshooa akizingua rasmi Chanjo hiyo amesema serikali kwa kutambua umuhimu wa zao la Mifugo ileteta chango hiyo ili kuwaepusha wafugaji na magonjwa yanayozuilika, huku akiwasihi wafugaji wote ndani ya Manispaa ya Shinyanga kujitokeza kufikisha Mifugo yao Katika vituo vya uchanjaji ili kuwakinga na magonjwa nyemelezi kwa Mustakabari wa Halmashauri na taifa kwa Ujumla.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga