- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
BARAZA LA WAZEE WA MANISPAA YA SHINYANGA LAWAPONGEZA MSTAHIKI MEYA NA MKURUGENZI WA MANISPAA
Na. Shinyanga MC.
Baraza la Wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kauli moja limewapongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko kwa niaba ya Waheshimiwa Madiwani wote na Ndg. Jomaary Satura kwa niaba ya watumishi wote wa Manispaa kwa utendaji kazi wao bora katika nyanja mbalimbali ikiwamo kuongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akisoma baadhi ya mafanikio kwa uongozi huo ni pamoja na kupandisha ukusanyaji wa mapato mara mbili zaidi ya awali, kuimarisha nidhamu kwa watumishi na katika matumizi ya fedha za Serikali, uboreshaji wa miundombinu ya ufanyaji biashara na uwezeshaji wananchi kiuchumi elimu, afya pamoja na kuboresha mazingira na upendeshaji wa mji wa Shinyanga kwa ujumla wake.
Hayo yamesemwa leo terehe 28 Aprili, 2023 na Katibu wa Baraza la Wazee Ndg. Laurent Kashindye wakati wa ikisoma Risala ya Wazee kwa wajumbe wa baraza na uongozi wa Manispaa wakati wa mkutano huo ambao pamoja na wajumbe wake wa Manispaa lakini pia alikuwepo Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Shinyanga mzee Faustine Sengerema.
Akifungua Mkutano huo na kutoa salamu za wazee, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa mzee Stephano Tano alisema kuwa Baraza la Wazee linaridhishwa na kufurahishwa sana na mwenendo wa utumishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Ndg. Jomaary Satura na wasaidizi wake wote kwa namna ambavyo wanaiheshimisha Manispaa kitaifa, katika ubunifu wake na utekelezaji wa mipango yao kisasa zaidi, na Mstahiki Meya Mhe. Elias Masumbuko na Waheshimiwa Madiwani kwa usimamizi ulio bora kabisa kwa Menejimenti hata sasa wameifanya Manispaa kuwa ya kuigwa na Halmashauri nyingine.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Shinyanga mzee Faustine Sengerema alisema kuwa, kuzinduliwa rasmi kwa Baraza hilo kunakwenda kuimarisha na kutambua thamani ya wazee kwa Manispaa kwakuwa sasa wataanza kushirikishwa rasmi kayika ngazi mbalimbali za maamuzi na vikao rasmi kama vile Baraza la Madiwani, Kamati za Maendeleo za Kata na vikao rasmi vya kila mwaka ambavyo vimetamkwa katika muongozo wa uanzishwaji wa mabaraza ya wazee.
Akitoa salamu kwa niaba ya Manispaa ndg. Satura alisema kuwa katika utekelezaji wake wa shughuli za kila siku, Manispaa inaheshimu sana, inatambua na kuthamini michango na uwepo wa wazee katika Manispaa huku akiwaomba ushirikiano zaidi na kwamba milango ipo wazi Manispaa na wanakaribishwa wakati wowote.
Aidha Mstahiki Meya Mhe. Masumbuko aliwaeleza wazee kuwa yeye na Baraza zima la Manispaa wanapokea ushauri wote uliotolewa, wataufanyia kazi na kwamba waheshimiwa madiwani wanawategemea sana wqzee katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
MATUKIO KATIKA PICHA
Picha ikionesha baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wazee Manispaa ya Shinyanga wakifuatilia kikao
Mshtahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akielezea jambo wakati wa kikao
Picha ikionesha baadhi ya wajumbe wakiwapongeza viongozi wa Manispaa akiwamo Mkurugenzi wa Manispaa ndg. Jomaary Satura mwenye shati nyeupe.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga