- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga leo tarehe 27 Oktoba, 2023 imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika ziara hii Naibu Meya Mhe. Zamda Mwebea ameeleza kwamba lengo la ziara ni kukagua na kuona namna ambavyo miradi hiyo inavyoendelea kutekelezwa huku akiwapongeze wasimamizi wa miradi hiyo na kuwataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi kwa kuzingatia ubora mzuri wa majengo kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa.
"Baraza la Madiwa kwa ujumla tunawapongeza kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo niwaombe wasimamizi kuendelea kusimamia thamani za vitu vyote na niwatake mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili yote yakamilike kwa wakati na yaanze kutumika"amesema Mhe. Mwebea
Awali, Baraza la Madiwa limetembelea miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari Ngokolo B , ujenzi wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana Shinyanga, ujenzi wa jengo la dharula EMD katika Hospital ya Manispaa ambao umekwisha kamilika pamoja na ujenzi wa soko kuu ambapo jumla ya vyumba 41 vya chini vipo tayari kwa ajili ya kutumika na baadhi ya wafanyabiashara wameshaanza kufanya biashara katika vyumba hivyo.
Lengo la ziara hii ni kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo ili kutoa ushauri wa mambo mbalimbali katika utekelezaji wa miradi na kujua ni hatua ipi imefikia kwa kila mradi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga