- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Viongozi wa Vyama vya Siasa pamoja na Wadau wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wamekutana na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Shinyanga Mjini Mwl. Alexius Kagunze kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni Pamoja na kuwakumbusha kuweka mawakala wao katika vituo vya kujiandikishia kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 21 hadi 27, 2024.
Akizungumza kwenye kikao hiki leo Agosti 16, 2024 Mwl. Kagunze amesema lengo la kikao hiki ni kuwakumbusha vyama vya siasa kuwa wanao wajibu na haki ya kuweka mawakala wao katika vituo vya kujiandikishia kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura Pamoja na kuwahamasisha wanachama wao kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
“Hivi karibuni kuanzia tarehe 21 hadi 27 tutakuwa na uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ni vema sasa tumeona tuwashirikishe wadau na viongozi wa vyama vya siasa vyote ili kuhamasisha wanachama na wafuasi wenu waweze kujiandikisha,kuhakiki na kuboresha taarifa zao kwa muda uliowekwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi vilivyopo katika jimbo letu” Amesema Mwl. Kagunze.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura katika Jimbo la Shinyanga Mjini litaanza rasmi Agosti 21 mpaka 27 ,2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga