- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Tuesday 6th, June 2023
@KATA YA LUBAGA
Wananchi wa mtaa wa azimio katika hali isiyokuwa ya kawaida wameshindwa kuvumilia kusubiri bajeti ya Serikali katika kuwatimizia kilio chao cha siku nyingi cha uhaba wa maji hatimaye wameamua kuungana pamoja kwa uzalendo wao wakishirikiana na ofisi ya mtendaji wa kata ya Lubaga Pamoja na Walezi wa kata ndg. Lenard Chepe na Boniphace Marago kujitolea kuchimba mtaro wa bomba la maji upatao km 5.22 ili waondokane na adha ya maji waliyokuwa nayo zaidi ya miaka 40.
Uongozi wa Chama wilaya ya shinyanga -manispaa wakiongozwa na mheshimiwa mwenyekiti wa CCM. Abubakari GulamHafeez Mukadam Wakishirikiana katika zoezi hilo kwa kutoa hamasa kwa wananchi na kuunga mkono juhudi zao na kushiriki katika uchimbaji wa mtaro pamoja na kuwafuta jasho kwa kiasi cha sh 3,000,000/= (milioni tatu) kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa hali kadhalika ofisi ya mstahiki Meya iliahidi kuwafuta kwa kiasi cha sh.1,500,000/=(Milioni moja na laki tano). pia uongozi wa CCM kata ya Ndembezi iliahidi kutoa sh.100,000/= (laki moja) Ambapo sh 50,000/= (elfu hamsini) ilitangulizwa papo hapo.
Aidha Mtendaji wa kata ya Lubaga Ndg Lucas Venance Nkelege Aliwashukuru wananchi na wadau walioshiriki katika zoezi hilo na kuomba wadau wazidi kujitokeza kuonyesha uzalendo na kuunga mkono juhudi za Wananchi wa Azimio,pia alimuomba Mwenyeketi (Mgeni rasmi) Pamoja na Mstahiki Meya kufanya harambee ndani ya Manispaa ikihusisha Chama cha Mapinduzi (CCM) ,ofisi ya Mkurugenzi na wadau wengine ili kiasi kitakacho patikana kiweze kutatua au kupunguza tatizo la maji ndani ya manispaa nzima ya Shinyanga na sio ndani ya lubaga tu.
Harambee hiyo inatarajiwa kukusanya zaidi ya shilingi Milioni mia moja (100,000,000/=)
Ofisi ya Afisa Mtendaji kati ya Lubaga inasema ‘’Shinyanga Manispaa tunaweza Maji ni haki ya kila mtu na Hatungoji bajeti ya serikali,tunatimiza sasa kuunga juhudi ya Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Raisi wa Tanzania Mh. John Pombe Joseph Magufuli’’
Kwa pamoja tuunge mkono harambee hii kubwa ya kihistoria ya maji katika Manispaa yetu ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0767042958
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga