- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga kunufaika na mradi wa ALAT Taifa kwa kushirikiana na UN-WOMEN utakaosaidia kutokomeza ukatili na unyanyasaji dhidi wanawake na watoto
Akiongea katika warsha iliyofanyika katika ukumbi wa Kalinjuna Manispaa ya Shinyanga,Mwenyekiti wa ALAT Taifa Mstahiki Meya Gulamhafiz Mukadam amesema kuwa mradi huo utajikita katika kutatua tatizo la unyanyasaji na ukatili kwa wanawake na watoto uliokithiri mkoani humo.
Gulamhafiz ameongeza kwa kusema kuwa tabia na mazoea kwa baadhi ya wanaume kutoa lugha chafu za kuzalilisha katika maeneo ya masoko,bar,Shule na taasisi mbalimbali za umma ni ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Aidha Regional Program Manager For East and Southern Africa UN-WOMEN ,Dr.Sadiq Syed amesema kuwepo kwa ubunifu na njia mpya za kujiinua ki uchumi kutasaidia kujenga usawa wa kijinsia na kuhakikisha kunapatikana maendeleo endelevu katika kuhamasisha ushiriki wa kina mama katika shughuli mbalimbali.
Naye Mwezeshaji Mwajina Lipinga wa OR-TAMISEMI amesema mradi huo utawanufaisha wanawake kwa kuimarisha uchumi wa kaya,kuodoa mila na desturi kandamizi,kuimarisha mahusiano na malezi katika kaya,Utekelezaji na usimamizi sahihi wa kisheria ,huduma kwa waathirika wa ukatili,mazingira salama shuleni na stadi za maisha,pamoja na uratibu, ufatiliaji na tathmini .
Vilevile Mratibu wa mradi kutoka ALAT Taifa bi.Christina Emmanuel ameongeza kuwa mradi huo utasaidia kupunguza na hatimaye kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa kubainisha aina ya ukatili ambapo alisema kuna ukatili wa kingono,wa kimwili,kisaikolojia na kiuchumi na kusistiza kuwa mradi huo utatekelezwa kwa ufanisi ili kumaliza kabisa tatizo hilo.
Pia mwezeshaji kutoka UN-WOMEN Lucy Tesha amesema ushirikiano baina ya UN-WOMEN pamoja na serikali za mitaa na tawala za mikoa utachochea zaidi kwa mwanamke kupewa kipaumbele katika kufanya maamuzi,kusikilizwa,kupata taarifa mbalimbali za kijamii na kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Aidha baadhi ya wajumbe katika warsha hiyo wamewataka wanawake kuvaa mavazi yanayositiri vema miili yao ili kutounda mazingira yatakayopelekea kufanyiwa vitendo vya uzalilishaji.Pia washiriki wameomba kuwepo kwa dawati la jinsia katika masoko kwa lengo la kushughulikia unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika maeneo hayo
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga