- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA YA MANISPAA YA SHINYANGA YAFANYA ZIARA YA KUKAGUA NA KUTEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO.
Na. Shinyanga Mc
Kamati ya Fedha na Utawala ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Naibu Meya wa Manispaa Mhe. Zamda Mwebea leo tarehe 17 Aprili, 2024 wametembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, ujenzi wa madarasa 2 katika shule ya msingi Kolandoto, ujenzi wa Zahanati ya Mwamagunguli Kolandoto, ujenzi wa vyumba viwili vya maabara katika sekondari ya Mwangulumbi pamoja na ukamilishaji wa vyumba 4 katika shule ya sekondari Masekelo.
Pamoja na mambo mengine kaimu mwenyekiti wa kamati ya fedha na Utawala Mhe. Zamda Mwebea kwa niaba ya Baraza zima la Madiwa wa Manispaa amewapongeza wasimamizi wote wanaosimamia miradi hii na kuwaomba kuendelea kusimamia kwa umakini kwa kuzingatia kiwango bora katika majengo na kujenga majengo yenye kuendana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali.
Lengo la ziara hii ni kuangalia hatua ipi imefikia ya utekelezaji wa Miradi pamoja na kutilia nguvu pale palipokuwa na changamoto na kutoa ushauri wa mambo mbalimbali.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga