- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Waalimu kutoka shule zenye kidato cha tano na sita wapatiwa mafunzo ya uelewa juu ya mtaala mpya wa kidato cha tano na sita, ambapo mafunzo hayo wameanza kupatiwa jana tarehe 5 Julai, 2024 katika ukumbi wa shule maalum Buhangija Shule ya msingi iliyojumisha halmashauri 3 ikiwemo halmashauri ya Manispaa ya shinyanga, halmashauri ya shinyanga pamoja na halmashauri ya kishapu.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Mkurungenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius kagunze huku akiwataka walimu kujifunza kwa umakini ili wakalete mabadilika katika sekta ya elimu ya sekondari ya juu.
Mtaala huo mpya tayari umeanza kutumika kwa kidato tano kilichoanza Julai, 2024, ambapo moja ya masomo ambayo yamebadilika ni somo la civics ambalo kwa sasa litatambulika kama somo la historia ya Tanzania na Maadili huku somo la commerce likitambulika kama business studies ( elimu ya biashara).
Mafunzo hayo ya kujengewa uelewa wa pamoja yanahusisha shule zote zenye kidato cha tano na sita kwa serikali na shule binafsi na yanatarajia kumalizika kesho tarehe 6 Julai, 2024
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.