• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

WAJASIRIAMALI, TUMIENI FURSA VIZURI - RC MACHA

Posted on: September 9th, 2024


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamiringi Macha amewataka wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za ngozi katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutumia vizuri fursa za upatikanaji wa ngozi kutokana na machinjio ya wanyama yaliyopo Mkoa wa Shinyanga kutengeneza bidhaa nyingi zaidi na hivyo kukuza uchumi wa Taifa.


Ameyasema hayo leo tarehe 9 Septemba, 2024 wakati akifungua mafunzo ya wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa za ngozi Manispaa ya Shinyanga ambayo yanaratibiwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) yanafanyika kwa siku (2) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka TAMISEMI, SIDO, TBS, wadau nk huku akisisitiza ubunifu zaidi.


“Ningependa kuwaasa mjitahidi kutumia vizuri fursa za upatikanji wa ngozi kwa sababu ndani ya Mkoa wa Shinyanga kuna machinjio ya wanyama mbalimbali kama ng’ombe, mbuzi na kondoo ambayo kupitia machinjio haya mnaweza mkapata kiasi kikubwa cha ngozi na mkafanikiwa kutengeneza bidhaa nyingi zaidi na kupata faida kubwa hatimaye kukuza uchumi wetu na Serikali pia kuongeza pato lake hapo,” amesema RC Macha.


Kwa upande wake meneja wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kitengo cha Tafiti na Mafunzo Mwl. Hamisi Mwanasala amesema mafunzo haya yamelenga kuwafikia wajasiriamali takribani 40 wanaojishughulisha na bidhaa za ngozi na amewataka washiriki wote kutumia vyema mafunzo haya ili kuboresha bidhaa wanazozalisha ziendane na viwango vya TBS.


“Mafunzo haya yamekusudia kuwasaidia wajasiriamali wanaojishughulisha na bidhaa za ngozi takribani 40 ili waweze kuboresha bidhaa zao za ngozi ziendane na viwango ambavyo Shirika la Viwango Tanzania limethibitisha ili kukuza soko la ngozi nchini” amesema Mwl. Hamisi.


Mafunzo haya ya wajasiriamali yatafanyika kwa siku mbili kuanzia leo Jumatatu tarehe 9 Septemba, 2024 hadi tarehe 10 Septemba, 2024 mafunzo ambayo yanatajwa kuwa yenye tija zaidi kwani yatawaongezea ujuzi na maarifa na kwenda kuinua uchumi wao na wa Taifa kwa ujumla.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.