- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Shule ya Sekondari Ndala ni moja ya Shule za Serikali Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga zilizofanya vizuri Katika mitihani ya kidato Cha nne pamoja na mtihani wa upimaji kidato Cha pili kwa Mwaka wa masomo 2024 hali iliyopelekea uongozi wa shule hiyo kuwapongeza waalimu wa masomo mbalimbali yaliyofanya vizuri kama sehemu ya kutambua jitihada na mchango wao Katika kufikia ndoto za wanafunzi.
Vyeti hivyo vya Pongezi vimetolewa leo Februari 27, 2024 na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma Sekondari Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Richard Makoye, ambaye amewapongeza walimu, bodi ya Shule, kwa kufanya vizuri Katika mitihani hiyo huku akiwataka kuongeza kasi zaidi Katika ufundishaji ili shule hiyo iweze kufanya vizuri Katika ngazi ya Taifa kwa Mwaka wa masomo 2025.
"Kazi nzuri iliyofanywa na walimu hawa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Tumeridhishwa lakini, kitu alichoniagiza Mkurugenzi wetu ni kuwataka walimu kuongeza juhudi zaidi anatambua jitihada zenu lakini anahitaji ufaulu wa daraja la kwanza, pili na daraja la tatu pekee, kwa sababu shule inamiundombinu mizuri, bora na rafiki kwa wanafunzi kufikia malengo yao". Amesema Mwl. Makoye
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Mwl. Marco Itenga amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa ushirikiano mkubwa anao toa kwa walimu wa Shule zote za Sekondari huku akiahidi kuwa Shule hiyo kwa Mwaka wa masomo 2025 itakwenda kufanya vizuri zaidi Katika mitihani ya taifa ili kuendelea kutetea heshima yao ya kuwa miongoni wa Shule za Serikali zinazofanya vizuri kitaaluma.
Ikumbukwe kuwa Shule ya Sekondari Ndala imeshika nafasi ya 3 kati ya shule 21 kwa shule za Serikali Katika matokeo ya kidato Cha nne kwa ufaulu wa jumla ya 95% kwa Mwaka 2024 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2023 ambapo ufaulu wa jumla ilikuwa 90% , upimaji kidato Cha pili imeshika nafasi ya 1 kati ya Shule 21 za manispaa ya shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.