- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
SALAMU ZA SHUKRANI
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mhe. Anamringi Macha kwa utumishi wake uliotukuka akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Mheshimiwa Macha, katika kipindi chako cha uongozi, tumeona dhamira yako ya kweli ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa shinyanga. Umekuwa kiongozi mwenye maono, aliyejitoa, na uliyeweka mbele maslahi ya wananchi. Kwa kuhamasisha uwajibikaji, mshikamano, na nidhamu ya kazi katika ngazi zote za utawala, jambo ambalo limeleta mabadiliko chanya katika sekta mbalimbali
Tunathamini sana mchango wako katika kuimarisha utawala bora, kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kuhimiza ushirikiano baina ya viongozi na wananchi. Umeacha alama isiyofutika katika historia ya Mkoa wa Shinyanga.
Tunakuombea afya njema, maisha marefu, na mafanikio katika majukumu yako mengine ya sasa na ya baadaye. MANISPAA YA SHINYANGA TUTAENDELEA KUKUKUMBUKA KAMA KIONGOZI MWADILIFU, MWENYE HEKIMA NA BUSARA.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.