- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
RC MNDEME AWATEMBELEA WALIOKUBWA NA MAAFA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 6 Novemba, 2023 amewatembelea wahanga wa maafa walioezuliwa na kubomolewa makazi yao katika kata ya Kizumbi kitongoji cha kashanda kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.
Akizungumza na wahanga hao Mhe. Mndeme amewapa pole wahanga wote huku akiwataka kuendelea kuchukua tahadhari za mvua kali zinazoendelea kunyesha kwa kuhama mabondeni na kwenye nyumba ambazo haziwezi kuhimili mvua kubwa .
"Niwape pole wahanga wote lakini pia pokeeni salamu za pole na upendo kutoka kwa Rais wetu Dkt. Samia pia niwaombe mtoke kwenye mazingira hatarishi ili kuepuka madhara makubwa zaidi" amesema Mhe. Mndeme
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mndeme ametoa maagizo kwa mkuu wa wilaya kufanya tathmini ya chakula kwa kaya zote zilizopoteza chakula na makazi ili waweze kupatiwa msaada.
Jumla ya kaya 27 zimepoteza makazi ambapo nyumba 31 zimeezuliwa na kubomoka.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.