- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
MWL. KANGUNZE ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Na. Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 31 Mei, 2024 amefanya ziara ya kukagu na kutembelea miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ndani Manispaaa ya Shinyanga huku akiwa ameambatana na wataalam.
Mwl. Kagunze ameweza kutembelea mradi wa ujenzi wa zahanati ya mwamagunguli iliyopo katika kata ya kolandoto, ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya awali na msingi kolandoto , ujenzi wa bwalo na jengo la utawala katika shule ya wasichana shinyanga pamoja na ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD katika hospitali ya Manispaa huku akiwasihi mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ila wanufaika wa miradi hii waanze kuitumia.
“Naomba muongeze kasi ya ujenzi lakini ujenzi uwe wenye ubora na unaojali thamani ya pesa ya serikali ili wanufaika wa miradi hii waanza kuitumia.” amesema Mwl. Kagunze
Pamoja na mambo mengine Mwl. Kagunze amewataka wasimamizi wa miradi hii kuendelea kupanda miti kwa wingi ili kutunza mazingira na kupendezesha mazingira yanayozunguka miradi hii.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.