- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
MWL KAGUNZE AWAONYA WANAOKWEPA KULIPA USHURU MNADA WA OLD SHY.
Na.Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Halmashari ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amewaonya wale wote wenye tabia ya kukwepa kulipa ushuru na wale wanaokuwa na tabia ya kutorosha mifugo katika mnada wa Old shinyanga.
Hayo ameyasema leo tarehe 23 Julai, 2023 alipotembelea mnada huo kwa lengo la kuona namna ambavyo shughuli za mnada zinavyotekelezwa, na baada ya kufika eneo hilo alibaini baadhi ya watu wasiokuwa wazalendo wakiwa katika harakati za kutaka kutorosho mifugo kutoka eneo la mnada baada ya kuwa wamenunua huku baadhi wakiwa wametoka eneo hilo bila kulipa ushuru jambo ambalo limempelekea Mwl.Kagunze kutoa onyo na kuagiza kuimarishwa kwa udhibiti wa makusanyo ya mapato eneo hilo.
“Nitoe onyo kwa wale wote wenye tabia isiyo ya kizalendo ya kukwepa kulipa ushuru na wale wanaotorosha mifugo eneo hili waache kwakuwa serikali ipo kazini muda wote, na atayebainika atachukuliwa hatua za Kisheria,” amesisitiza Mwl.Kagunze.
Mnada wa Old Shinyanga ambao hufanyika kila jumapili ni maarufu kwa uuzaji na ununuzi wa mifugo mbalimbali ambapo inakadiriwa Zaidi ya mifugo 1800 ikiwamo ng’ombe, Mbuzi na Kondoo hupelekwa eneo hilo.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.