- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
MWL. KAGUNZE ATEMBELEA SHULE YA WASICHANA SHINYANGA
Na. Shinyanga Mc
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 3 Septemba, 2023 ametembelea Shule ya Sekondori ya Wasichana Shinyanga iliopo Kata ya Ndembezi Mtaa wa Butengwa.
Mwl. Kagunze amefika shule hapo kwa lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa miundombinu mbalimbali ambayo bado ipo katika hatua ya ukamilishaji na kuwataka mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha kwa wakati kwa sababu kila kitu kipo.
"Naomba muongeze kasi ya ujenzi ili majengo ambayo hayajakamilika yakamilika kwa wakati kwani mwakani tunategemea kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza " alisema Mwl Kagunze
Pamoja na Mambo mengi Mwl. Kagunze alipata wasaa wa kutembelea, kukagua na kuelekeza ukamilishwaji wa haraka wa nyumba za walimu katika Shule ya Sekondari Lubaga ili nyumba hizo zianze kutumiwa.
Ziara hii ya Mwl. Kagunze ni muendelezo wa ziara zake kwa lengo la kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.