- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
MWL KAGUNZE ARIDHISHWA NA UJENZI MADARASA YA BOOST
NA. SHINYANGA MC
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze ameridhishwa na ujenzi wa Madarasa ya BOOST yanayoendelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa ziara Mwl. Kagunze amezitaka kamati za shule kuendelea kutunza samani za shule ,nyaraka za ujenzi, kufuata taratibu na miongozo ya manunuzi,kutunza miti iliyopo na kupanda miti mingine ili kuendelea kupendezesha maeneo yote yanayozunguka shule.
‘’Nimeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa Madarasa ya BOOST hii inaonesha Dhahiri tunajua umuhimu wa Elimu katika hili nizitake kamati zote kutunza Samani, nyaraka za Ujenzi, kufuata taratibu na miongozo ya manunuzi, kutunza miti iliyopo na muongeze kupanda miti mingine ili kupendesha shule zetu’’ alisema Mwl. Kagunze
Pamoja na mambo mengine Mwl. Kagunze alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha sekta zote hususani elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.