• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MWL. KAGUNZE AFANYA KIKAO KAZI NA WATENDAJI WA KATA, MITAA NA VIJIJI MANISPAA YA SHINYANGA

Posted on: October 20th, 2023

MWL. KAGUNZE AFANYA KIKAO KAZI NA WATENDAJI WA KATA , VIJIJI NA MITAA MANISPAA YA SHINYANGA.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 20 Oktoba, 2023 amefanya kikao kazi na Watendaji wa Kata, Mitaa pamoja na Vijiji katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna ulipo katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza katika kikao Mwl. Kagunze amewapongeza watendaji kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo pamoja na kusimamia vizuri majukumu ya kila siku katika sehemu zao za kazi.

"Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika maeneo yenu ya kazi pamoja na usimamizi mzuri katika kuhudumia wananchi " alisema Mwl. Kagunze

Aidha, Mwl. Kagunze amewaagiza watendaji kwenda kusimamia kwa ukaribu mambo mbalimbali yakiwemo kutenga siku moja ya wiki ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kufanya mikutano ya hadhara kila mwezi kwa kuwasomea mapato na matumizi katika maeneo yao ya kiutawala pamoja na kutoa taarifa ya utekelezaji wa vikao na mikutano iliyofanyika kila mwezi.

Pia amewataka kwenda kusimamia usafi na utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti na kulinda miti iliyokwisha pandwa, kusimamia mapato ya ndani, kudhibiti utoro kwa wanafunzi, kusimamia ulaji wa chakula mashuleni, kusimami miradi ya maendeleo, kutoa taarifa za fedha zinapoingia kwenye akaunti za kata kwa ajili ya miradi kwa wananchi pamoja na kuendelea kutoa taadhari ya mvua ya El Nino kwa wananchi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga Ndg. Said Kitinga pia amewataka watendaji kufahamu na kufuatilia kila miradi inayoendelea kutekelezwa katika kata zao pamoja na utoaji wa taarifa uzingatie ngazi za kiutawala.

Pamoja na mambo mengi Mwl. Kagunze alipata wasaa wa kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za watendaji ambazo waliziwasilisha na nyengine alizichukua kwa ajili ya kuzifanyia kazi.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.