• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA SHINYANGA DAVID NKULILA AFARIKI DUNIA.

Posted on: August 23rd, 2021

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Mathew Nkulila (57) ambaye ni Diwani kata ya Ndembezi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatatu Agosti 23,2021 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.


Nkulila amekuwa Diwani wa kata ya Ndembezi tangu mwaka 2010 na Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mwaka 2010-2015.


Nkulila alichaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Novemba 24 Mwaka 2020 na ametumikia nafasi ya Meya kwa kipindi cha miezi 10 hadi umauti ulipomkuta.


David Mathew Nkulila alikuwa na maono ya kuifanya Manispaa ya Shinyanga kuwa Jiji.


 Nkulila atakumbukwa kwa misimamo yake thabiti katika kutetea wanyonge, asiyekubali kuyumbishwa na kupiga vita rushwa na ufisadi. 


Msiba upo nyumbani kwake mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi jirani na Kanisa la Moravian, taratibu za ratiba za mazishi tutawataarifu.



Historia fupi ya Marehemu David Nkulila 


David Mathew Nkulila alizaliwa tarehe 16/04/1964, Tabora mjini, mkoa wa Tabora.


David Mathew Nkulila alianza darasa la kwanza katika shule ya Msingi Bunda mwaka 1974, na baadae Shule ya Msingi Mkendo mwaka 1975, alihamia Shule ya Msingi Old Shinyanga mwaka 1976 na baadaye Shule ya Msingi Mwenge-Shinyanga  mwaka 1977 hadi alipohitimu darasa la saba mwaka 1980 katika shule hiyo.


Baba yake mzazi na Marehemu Nkulila alikuwa mtumishi wa serikali hali iliyopelekea Marehemu Nkulila kuhama Shule moja kwenda nyingine ili kumfuata baba yake sehemu alipohamishiwa.


Marehemu David Mathew Nkulila alipata elimu yake ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya Kilimo Kilosa (Kilosa Agricultural Secondary School) kati ya mwaka 1981-1984. Shule hii ya Sekondari ya Kilimo Kilosa ni maarufu hapa nchini kwa kauli mbiu yake ya "Elimu na Kazi"


Baada ya kuhitimu kidato cha nne Marehemu Nkulila alijiajiri na kazi ya Kilimo ambayo ndiyo ilikuwa kazi yake ya msingi hadi mauti yalipomkuta leo 23/08/2021.


Historia yake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na majukumu ya kisiasa


Marehemu David Mathew Nkulila ana uzoefu wa kutosha katika masuala ya siasa. Marehemu Nkulila alijiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM) mwaka 1995. Ndani ya CCM Marehemu Nkulila amewahi kushika nyadhifa mbalimbali.


⏩ Marehemu Nkulila amewahi kuwa mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya ya Shinyanga Mjini kati ya mwaka 2013-2017


⏩ Katibu wa CCM Kata ya Ndembezi kati ya mwaka 2007-2012.


⏩ Katibu wa CCM Kata ya Ngokolo.


⏩ Katibu wa CCM Tawi la Bugoyi kati ya mwaka 2003-2007.


Nafasi alizozitumikia


⏩ Marehemu Nkulila amekuwa Diwani wa Kata ya Ndembezi kwa vipindi vitatu mfululizo toka mwaka 2010 hadi leo tarehe 23/08/2021 mauti yalipomkuta.


⏩ Marehemu Nkulila amekuwa Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kati ya mwaka 2013-2015.


⏩  Marehemu Nkulila amekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Mabambasi kati ya 2004 - 2019.


⏩ 2000-2003 Mwenyekiti wa kamati ya WES mtaa wa Mabambasi.


⏩  Amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) kwa zaidi ya miaka 10.


Kazi alizozifanya akiwa Diwani wa Kata ya Ndembezi


Marehemu David Mathew Nkulila kwa kipindi chake chote akiwa kama diwani wa Kata ya Ndembezi alifanikiwa kuwawakilisha vema kwa uadilifu mkubwa wakazi wa Kata ya Ndembezi.


(a)Alisimamia upimaji wa ardhi (viwanja) katika Mitaa ya Ndembezi na Butengwa. Awali mitaa hii ilikuwa na hadhi ya vijiji na ardhi ilikuwa haijapimwa.


(b) Alisimamia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara katika viwango vya lami na changarawe ikiwemo mitaro, makalvati, vivuko na madaraja.


(c) Alisimamia ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyopo katika mtaa wa Butengwa.


(d)Alisimamia ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Ndembezi iliyopo katika mtaa wa Butengwa. Kwa sasa ujenzi huo upo katika hatua ya boma. Eneo hili la ujenzi wa Zahanati lilipatikana kufuatia juhudi zake akishirikiana na ofisi ya Mtendaji wa kata ya Ndembezi.


(e) Alisimamia utolewaji wa mikopo ya bila riba inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutoka 10% ya mapato yake ya ndani kwa makundi ya vijana, wanawake na walemavu.


Mambo aliyoyapenda (Hobby)


Marehemu Nkulila alipenda kusoma vitabu, majarida na magazeti, Mitandao ya Kijamii na alipenda sana kuendesha baiskeli.

R.I.P Mstahiki Meya Nkulila

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.