• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MKUU WA WILAYA AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI MANISPAA YA SHINYANGA KUADHIMISHA MIAKA 60 YA UHURU

Posted on: November 26th, 2021

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imezindua Kampeni ya upandaji wa miti ya matunda na vivuli kuelekea katika maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, na miaka 59 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni nyenzo moja wapo ya kukabiliana na madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Uzinduzi huo umefanyika Novemba 20,2021 katika viwanja vya machinjio ya ng’ombe ya Kisasa kata ya Ndembezi ambao umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko na kuhudhuriwa na viongozi na wakuu wa taasisi na Idara mbalimbali za serikali na zisizo za kiserikali, wadau wa maendeleo pamoja na wakazi wa manispaa ya Shinyanga, ambapo jumla ya miti 2,000 imepandwa na kugawiwa wakazi wa eneo hilo.

Akizindua kampeni hiyo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amewataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti na badala yake waitunze ili kupunguza kama si kumaliza madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, mfano kuongezeka kwa joto duniani.

“Tuendelee kuilinda miti tuliyoipanda kipindi cha nyuma, lakini pia tuendelee kupanda miti mipya, tuisimamie iote pamoja na kuhakikisha usalama wa miti ili mifugo isiharibu ili miti iwe imara” amesema Mboneko.

“Na safari hii Shinyanga tuna Kampeni yetu inasema Shinyanga ya miembe na mikwaju, miembe tunajua ni soko kubwa pamoja na mikwaju pia ina soko kubwa, kwa hiyo tutumie fursa hiyo ya utunzaji wa mazingira na kipato wakati mwingine, tuhakikishe tunapoadhimisha miaka 60 ya uhuru tutazame na mazingira yetu”, ameongeza Mboneko.

Mratibu wa Kampeni hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone amesema halmashauri hiyo imeweka malengo ya kupanda idadi ya miti ya matunda na vivuli milioni moja na laki tano, ambapo miti hiyo itagawiwa kwenye taasisi za umma na binafsi, shule za msingi na sekondari.

Kiwone amesema miche mingine ya miti itakabidhiwa kwa pamoja na wakazi wa manispaa ya Shinyanga ili kuunga mkono jitihada za serikali kukabiliana na ongezeko la joto duniani ambalo limesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Abubakar Mukadam amewataka wakazi wa Shinyanga kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii huku akimulika suala la upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.

“Ndugu zangu mnafahamu kila mwaka hali ya hewa inazidi kubadilika ninawaomba kuipa nguvu serikali kwa kushirikiana nayo, kila mmoja kuchukua jukumu la kupanda, kuitunza na kuisimamia miti ili kuleta unafuu wa hali ya hewa nzuri ambayo imeanza kutoweka”, amesema Mukadam.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura amewashukuru wananchi na wadau mbalimbali waliojitokeza katika upandaji miti huku akibainisha kuwa upandaji miti ni jukumu la kila mmoja katika jamii.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.