• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ATEMBELEA SOKO LA MBAO LA CHAMAGUHA PAMOJA NA SOKO LA MACHINGA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA

Posted on: September 15th, 2021

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga leo tarehe 15/09/2021 amefanya mkutano na wafanyabiashara wa soko la Chamaguha na soko la Machinga. Mkuu wa mkoa  aliongozana na Mkuu wa Wilaya, Mkurugerunzi wa Manispaa ya Shinyanga pamoja na Afisa Biashara, Afisa Maendeleo ya Jamii, Afisa Mipango Miji, Afisa Utumishi na Afisa TEHAMA.

 Mkutano ulifunguliwa na Mkuu wa Wilaya na baadaye kuwakaribisha wafanyabiashara kutoa changamoto zinazowakabili.

     Mwenyekiti Msaidizi wa soko la chamaguha alitoa  mojawapo ya changamoto ni miundombinu ya barabara kuwa mibovu na wakati wa masika kushindwa kutumika  hivyo kuomba kuboreshwa kwa wakati.hata hivyo Mwenyekiti huyo alimpongeza Mkurugenzi kwa kujitahidi kutatua changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili.

Mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga alipata nafasi ya kuzungumza na wafanyabiashara na  kuwashukuru kwa kuhama kutoka soko la Kambarage bila shuruti, aliwaambia kuwa lengo kuu la Serikali ni kufanya biashara zao kukua na kuwa chachu ya maendeleo ya Manispaa ya Shinyanga.

Vivyo hivyo Mkurugenzi aliwaahidi kuwapa ushirikiano katika ukuaji wa soko kwa kuboresha miundombinu kama vile kuongeza idadi ya vyoo ili kuweza kutosheleza mahitaji ya wafanyabiashara pamoja na wateja kwa idadi.

Aidha katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa alizungumza na wafanyabiashara na kuwashukuru kwa kukubali kuhama kutoka soko la Kambarage na kuhamia soko jipya la Chamaguha kwa kufuata ushauri wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwenye matumizi ya sera ya Diplomasia na Maelewano.

Mkuu wa Mkoa amemshukuru Mkuu wa wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga na viongozi wengine kwa kuweka mazingira sawa mpaka soko kuanzishwa.

 Pia Mkuu wa Mkoa amesema kwa kushirikiana na Manispaa ya Shinyanga amewaahidi wafanyabiashara hao kuendelea kuwaboreshea miundombinu ya soko hasa kwa kuanza na urekebishaji wa  barabara ili kuwe na mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.

Pia Mkuu wa Mkoa aliwahakikishia wafanyabiashara wote katika soko la mbao la Chamaguha kuwa eneo hilo ndilo litakalokuwa eneo pekee la kuuza mbao pamoja na bidhaa za mazao ya misitu.

Akiwa katika soko la Machinga lililopo kata ya mjini, Mkuu wa Mkoa alikutana na wafanyabiashara ambao pia alisikiliza kero zao ikiwa ni Pamoja na ukosefu wa maji, miundombinu mibovu ya barabara, vibanda vya wafanyabiashara kutokuwa na ubora na kuhofia changamoto kubwa wakati wa masika, pia waliomba kuwepo na mnada siku ya jumatano ya kila wiki.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa aliwapa moyo wafanyabiashara hao kwa kuahidi kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kutatua changamoto zao zote. Aliwaahidi kulitangaza soko hilo kuwa rasmi na kulifanyia ufunguzi.

Viongozi wa soko la Machinga waliwasisitiza wafanyabiashara wenzao kutimiza majukumu yao kwa kulipia vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ili kufanya kazi katika mazingira yasiyokuwa na bugudha ama usumbufu.

MATUKIO KATIKA PICHA


Soko la mbao Chamaguha

Mkuu wa Mkoa akisikiliza Wafanyabiashara

Wafanyabiashara wakisikiliza kwa makini

Mkuu wa Mkoa akitembelea soko la mbao

Soko la Machinga

Mkuu wa Mkoa akisikiliza changamoto za

Wafanyabiashara wa soko la Machinga

Mkuu wa mkoa akitembelea Soko la Machinga

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.