- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED na BSL SCHOOLS TANZANIA Ndg. Peter Frank (Mr BLack) ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya SHINYANGA TEACHERS’ NIGHT kwa niaba ya kamati ya maandalizi amemkabidhi Tuzo ya heshima ya uongozi kwa Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze leo tarehe 3 Aprili, 2024 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ambapo wamempongeza zaidi kwa ushirikiano na juhudi zake katika uongozi bora hususani katika sekta ya elimu.
Aidha , Ndg Frank ameeleza kwamba walimu wa Shinyanga pia watakua na ziara ya kwenda mbuga ya wanyama Serengeti tarehe 3 na 4 Agusti, 2024 ikiwa ni kuunga juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kukuza utalii Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Kagunze ameishukuru kamati ya SHINYANGA TEACHER’S NIGHT na kuwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ili kuendelea kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.