• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MKURUGENZI MANISPAA YA SHINYANGA AWAAGIZA VIONGOZI WA ELIMU KUHAMASISHA JAMII

Posted on: August 26th, 2023

Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu wakuu katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuhakikisha wanafunzi wote wa Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri hiyo wanapata chakula Shuleni kwa kuhamasisha wazazi na walezi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao  ili kuwapa utulivu wa kujifunza wawapo shuleni.

Maelekezo hayo yametolewa jana, Agosti 25, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwalimu Alexius Revocatus Kagunze wakati anaongea na Maafisa Elimu Kata na Wakuu wa Shule za Sekondari wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwenye Mkutano wa kawaida wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Manispaa ya Shinyanga uliofanyika katika Shule ya Sekondari Buluba mjini Shinyanga.

"Upatikanaji wa Chakula Shuleni ni moja ya utekelezaji wa KPI (vigezo vya upimaji) za mikataba yenu mliyojaza kwa ajili ya kusimamia taaluma shuleni. Chakula shuleni ni muhimu sana kwa ajili ya kuleta utulivu kwa mwanafunzi kujifunza anapokuwa darasani. Nawaagiza kuhakikisha mnaitisha vikao vya wazazi kuhamasisha wazazi kuwachangia watoto wao chakula shuleni." Alisisitiza Kagunze.

Kuhusu usafi na utunzaji wa mazingira, Kagunze amewaelekeza Wakuu wa Shule na Walimu wakuu kuhakikisha mazingira ya Shule zao yanakuwa safi muda wote na kukitumia kipindi hiki cha kiangazi  kuandaa mashimo ambayo watapanda miti ya kutosha pindi msimu wa mvua utakapoanza.

"Tumieni kipindi hiki cha kiangazi kuandaa mashimo kwa ajili ya kupanda miti mingi msimu wa mvua utakapoanza. Yaandaeni vizuri, mtie mbolea na inasisitizwa kuwa tupande miti ya matunda ya kutosha pamoja na ya kimvuli pia. Aidha, tuendelee kuitunza miti ambayo tumekwisha ipanda ili kutunza mazingira yetu." Aliongeza Kagunze.

Wakati huo huo, Mkurugenzi Kagunze amewataka viongozi wa elimu hususani Walimu wakuu na Wakuu wa Shule kujenga umoja, upendo na ushirikiano huku wakitenda haki kwa walimu wote wanaowaongoza katika Shule zao.

Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) ulianzishwa mwaka 2005 ukiwa na malengo ya kuwakutanisha Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania kwa lengo la kubadilishana uzoefu wa uongozi mashuleni. Kwa mujibu wa Katiba ya Umoja huo, muundo wake umegawanyika katika ngazi ya Halmashauri, Mkoa, Kanda na Taifa.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.