• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MKATABA WA MILIONI 300 WASAINIWA KATI YA MANISPAA NA VETA KWA AJILI YA UTENGENEZAJI WA MADAWATI 2500 KWA SHULE ZA MSINGI NA VITI NA MEZA 2500 KWA SHULE ZA SEKONDARI

Posted on: October 31st, 2021

Madawati 2500 kwa shule za msingi, viti na meza 2500 kwa shule za sekondari itawezesha wanafunzi wote kuanzia chekechea hadi Sekondari kukaa katika madawati.hii inakwenda sambamba na kumsapoti Rais wetu mama Samia ambae amekuwa na msukumo mkubwa katika utoaji huduma kwa jamii, ambapo sh trillion 1.3 zilizotolewa katika mpango wa covid19  Manispaa imepokea million 880 kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa 35 kwa shule za sekondari na madarasa 9 kwa shule shikizi.Katika kumuunga mkono mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Manispaa ya Shinyanga imetumia mapato yake ya ndani kutengeneza madawati 2500 kwa shule za msingi, viti na meza 2500 kwa shule za sekondari.ambapo Mwenyekiti wa Wafanyabiashara ndg Shuma alialikwa ili ashuhudie kuwa sehemu ya fedha wanayotoa wafanyabiashara kama kodi inatumika kwa ajili ya maendeleo. Utengenezaji wa madawati , viti Pamoja na meza utatoa fursa kwa wanafunzi Zaidi ya 50 wa VETA katika fani ya useremala na uchomeleaji  kujifunza kwa vitendo.

Mchakato wa kutengeneza madawati uliwashirikisha wanajamii wote na ulipitia michakato yote ya manunuzi na VETA wakaibuka kidedea kwa kuwa wao ndo walikuwa the lowest bider na pia wana miundo mbinu ya kisasa ya Serikali katika kufanya kazi hiyo.

Mkuu wa Chuo cha VETA ametoa shukrani zake kwa uongozi wa Manispaa kwa kukubali kufanya kazi Pamoja.

Mwenyekiti wa Kamati za Huduma, Uchumi, Elimu na Afya Mheshimiwa Nkwabi alifurahishwa na mkataba huo wa ujenzi wa madawati ambapo alisema ile ndoto ya kuwa wa kwanza kitaifa inaenda kutimia na ndoto ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuwa jiji pia inaenda kufanikiwa.” Mkuu wetu, zile ndoto za Halmashauri ya Shinyanga kuwa jiji zinaenda kutimia, tunapotoa ujinga sasa ni dalili njema kuwa tunaelekea kwenye mafanikio”. Alisema Mheshimiwa Nkwabi.Alimaliza kwa kutoa shukrani zake na kuahidi kuwa kamati itatoa ushirikiano mkubwa kwa Mkurugenzi Pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuhakikisha mikakati yote ya maendeleo inafanikiwa kwa ufanisi mkubwa.

Pia Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndg. Shuma Madulu alitoa shukrani zake kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya kwa kuonyesha uwazi katika masuala yote yahusuyo maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. “Nimshukuru Mkurugenzi, kwa sababu Wakurugenzi waliopita Shinyanga ni wengi lakini kwa utandawazi huu amekuja kutuonyesha wafanyabiashara kushuhudia na kutukumbuka kuwa nasi ni wachangiaji wakuu katika maendeleo kitu ambacho hapo nyuma hakikuwahi kufanyika. Naomba Mkurugenzi aendelee Pamoja na Mkuu wetu wa Wilaya ambae amekuwa akisisitiza maendeleo akiamini Maendeleo ndani ya Shinyanga yetu yanawezekana”. Alisema Ndg Shuma.

Aidha kwa nyakati tofauti, Afisa Elimu Msingi na Sekondari Walitoa shukrani zao za dhati hasa wakizingatia kuwa miradi hiyo inawalenga wao moja kwa moja.

Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mheshimiwa Makune alitoa shukrani zake kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia kwa kuleta fedha kwa ajili ya mipango ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kisha akapata wasaa wa kumkaribisha Mkuu wa Wilaya Bi Jasinta Mboneko ili aseme machache kabla ya tukio la kusaini mkataba kuanza.

Mkuu wa Wilaya alianza kwa kuipongeza Halmashauri kwa hatua nzuri na Madhubuti ya kuhakikisha Miundo mbinu ya darasani inaimarika na kwamba kila mwanafunzi anakaa kwenye dawati ili kufanya zoezi la kujifunza liwe Rafiki kwa wanafunzi na walimu pia alimpongeza Mkurugenzi Pamoja na Kamati za Huduma, Uchumi, Elimu na Afya kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta Maendeleo. “Tukiacha wanafunzi twende kwa Walimu kwa sababu na wao katika mazingira ya Ufundishaji lazima wakae sehemu nzuri, kwa kuzingatia hilo mimi binafsi kama mkuu wa Wilaya nimekwishaanza kupeleka Meza na viti katika baadhi ya shule”. Alisema Bi. Mboneko. Alisisitiza Walimu kutoa majaribio kila wiki ili kuwaandaa Watoto wasiogope mitihani na kuwafanya wapate ufaulu mzuri.  

Baada ya Hotuba fupi ya Mkuu wa Wilaya Mkataba ulisainiwa na pande zote.

Hafla hiyo fupi ya utiaji Saini mkataba huo ilifanyika katika ukumbi wa VETA tarehe 28 Oktoba 2021 Alhamisi huku ikishuhudiwa na Wataalamu kutoka Manispaa, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara, Mkuu wa Wilaya, Mstahiki Naibu Meya, Mwenyekiti wa Kamati za Huduma, Uchumi, Elimu na Afya na baadhi ya Watumishi kutoka VETA.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.