- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga katika kuhakikisha jamii inaondokana na umasikini imetoa mikopo ya asilimia kumi isiyo na riba, mikopo inayotolewa kupitia makusanyo ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Akikabidhi mikopo hii mgeni rasmi katika hafla iliyofanyika leo aprili 02, 2025 Mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro amewasihi wanufaika hao kurejesha mikopo hii kwa wakati ili iweze kunufaisha vikundi vingine.
“Uchukuaji wa mikopo ni hiyari lakini urejeshaji wa mikopo ni lazima na kwa wakati, mkurugenzi wetu chini ya watendaji wake wamefanya kila kitu Kuhakikisha jamii na wakazi wa manispaa wanaondokana na umasikini ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali kuu, fedha hizi zitumike kama mlivyoandika kwenye maandiko yenu ya miradi, rejesheni kwa wakati, ili wadogo zenu, ndugu zenu, wanashinyanga nao waweze kupata mikopo hii.” Wakili Mtatiro.
Akitoa Elimu juu ya namna ya kupata mikopo ya asilimia kumi Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga Bi. Nyanjula Kiyenze amesema kigezo kikubwa cha kupata mkopo huo wa asilimia 10 ni kikundi cha watu kuanzia watano kwa vikundi vya wanawake na vijana huku watu wenye ulemavu anaruhusiwa kukopa mkopo huo hata mtu mmoja.
Kwa upande wake Msitahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amesema mpaka sasa kwa mwaka fedha 2024/2025 mikopo hii imetolewa kwa awamu mbili ambapo awali ilitolewa jumla ya milioni 90,000,000 Kwa vikundi vitatu, huku kwa awamu ya pili jumla ya Milioni 225,879,500 zimetolewa kwa jumla ya vikundi 19 kutoka kata mbalimbali za Manispaa ya Shinyanga.
Penina Ezekiel, Razalo John na Isack Samwel ni baadha ya wanufaika wa mikopo hii wameishukuru serikali kuleta mikopo hii inayowasaidia kuondokana na mikopo kandamizi kama kausha damu sambamba na kuwaepusha kuwa ombaomba Kupunguza wimbi la vijana wasio na ajira huku wakisema mikopo hiyo watarejesha kwa wakati ili iweze kuwanufaisha vikundi vingine.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.