- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Naibu Meya wa Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda S. Shabani ameongoza maadhimisho ya siku ya wanawake kwa ngazi ya Halmashauri, maadhimisho yaliyofanyika katika kituo cha afya Kambarage ndani ya manispaa ya shinyanga, maadhimisho yaliyoambatana na uchangiaji damu, usafishaji wa mazingira katika kituo hicho pamoja na utoaji wa misaada mbalimbali katika wodi ya wazazi.
Akizungumza katika maadhimishio haya leo machi 03, 2025 Mhe. Mwebeya amewapongeza wanawake hao kwa umoja na ushirikiano walioonyesha, huku akuwasihi kuendelea kulea familia katika maadili ya kitanzania ili kujenza kizazi chenye maadili.
“Wanawake manispaa ya shinyanga mmeonyesha ushirikiano wa hali ya juu sana katika kuwasaidia wazazi wenzetu, rai yangu kwenu kama wazazi wenzangu twendeni tukalee familia zetu na Watoto wetu katika miiko, maadili ya kitanzania, Watoto hawa ndiyo vingozi wa kesho ndio mama walezi wa familia zao kwa badae hivyo twendeni tukatimize majukumu yetu.” Amesema Mhe Mwebeya.
Kwa upande wake Afisa maendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Nyanjula M. Kiyenze amesema kwa kutumbua changaoto za uzazi jumla ya Milioni 1,100,000/ imetumika kununua vitu hivyo, huku Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilaya ya shinyanga wakitoa mifuko mitano ya saruji ili kuunga mkono juhudi za ujenzi wa uzio katika kituo hicho.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kimkoa yanatarajiwa kuadhimishwa machi 06,2025 katika halmashauri ya wilaya ya Msalala huku yakiangozwa na kaulimbiu isemayo “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.