• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

Mfumo wa FFARS Kuboresha Utoaji Huduma kwa Wananchi

Posted on: September 22nd, 2017

Mkurugenzi wa Manispaa leo amefungua mafunzo ya mfumo wa kielektroniki wa uhasibu na utoaji taarifa unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS). Mfumo huu wa kielektroniki unasaidia utekelezaji wa utoaji wa rasilimali fedha moja kwa moja kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma kwa kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma.  "FFARS itawapatia nyie watoa huduma mfumo sanifu uliorahisishwa ambao utawawezesha kutunza taarifa za fedha zinazotolewa na zilizopo katika vituo vyenu.  FFARS itaweza kufuatilia matumizi ya fedha hizo katika kufikia malengo ya utoaji huduma na kuhakikisha yanaendana na sheria za manunuzi na utoaji taarifa. Taarifa hizi zitasaidia Serikali kuimarisha Mfumo wa Usimamizi wa Fedha za Umma na kuongeza uwazi, na hivyo watoa huduma wa afya kuwa na wajibu kwa jamii wanayoihudumia.". Alisema Mkurugenzi wa Manispaa.

Kuanzia Julai 1, 2017 Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania iliaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za Halmashauri.  Vituo vya kutolea huduma ambavyo vinapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na Hospitali za Wilaya.  Zoezi hili ni sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Wakufunzi wa mfumo wa FFARS na PlanRep kutoka Idara ya Afya, Fedha na Mipango (Ndugu Emmanuel, Divina Masali na Alex Mpasa) kutoka Ofisi ya Halmashauri ya Manispaa

Mfumo huu mpya wa kupatiwa Rasilimali Fedha unatoa motisha kwa vituo vya kutolea huduma za afya na kuongeza kipaumbele cha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuongeza usawa na uwazi.  Upelekaji wa Rasilimali Fedha moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma inahakikisha kuwa Fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa. Mkakati huu mpya wa kuboresha sekta ya afya ni msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Mafunzo ya Mfumo wa FFARS yamekusudia kuwawezesha watumishi katika vituo vya Sekta ya Afya na Elimu kupata ujuzi wa namna ya kutumia mfumo wa kielektroniki wa FFARS ambao ndio watumiaji wa mwisho wa mfumo wa FFARS katika  Vituo vya Afya, Zahanati na Shule za Msingi na Sekondari za Manispaa ya Shinyanga. Mafunzo haya yatahakikisha kuwa watoa huduma katika vituo wana ujuzi unaohitajika katika usimamizi wa fedha na kutoa  huduma bora kwa wananchi wote Tanzania na kwa jamii zenye uhitaji.

Baadhi ya washiriki wa Mafunzo kutoka katika vituo vya kutolea huduma 

Mfumo huu wa FFARS unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI); Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi; na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, pamoja na USAID.  Mfumo utatumika katika vituo vyote vya kutolea huduma ya afya na shule, na uhuishaji huu wa mfumo utarahisishia na kuongeza ufanisi katika mifumo ya Serikali ya Tanzania na kuboresha usimamizi na matumizi ya Rasilimali za umma.

Pamoja na mafunzo ya FFARS, pia watumishi watajifunza mfumo mpya na ulioboreshwa wa kupanga bajeti unaojulikana Planing and Reporting (PlanRep) ambao utaanza kutumika kuandaa bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2018/2019. Mfumo huu utapunguza gharama zilizokuwepo wakati wa uandaaji wa bajeti ya Halmashauri kama vile gharama za kutengeza vitabu vya bajeti, gharama za usafiri wa kupeleka bajeti katika ngazi ya mkoa na Wizarani. Kwa maana mfumo utaruhusu uandaaji wa bajeti na utumaji wa bajeti kielektroniki kutoka ngazi ya kutolea huduma hadi wizarani bila kuhitaji watumishi kusafiri.

Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), ni wa miaka mitano na unatekelezwa katika mikoa 13 ya Tanzania bara.  PS3 inafanya kazi katika sekta mbalimbali ili kuimarisha mifumo ya mawasiliano, utawala bora, fedha na rasilimali watu, hususani kwa jamii zenye uhitaji.



Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.