- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
MENEJIMENTI YA MANISPAA YA SHINYANGA YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO.
Na. Shinyanga Mc
Manejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Bi. Mary Maka leo tarehe 15 Februari, 2024 imefanya ziara ya kukagu na kutembelea miradi ya Maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga.
Menejimenti imefanya ziara hiyo ya kukagua na kutembelea miradi ya maendelea kwa lengo la kuangalia ni hatua gani ujenzi umefikia katika miradi hii huku menejimenti ikiwataka mafundi kuzidi kuongeza kasi ya ujenzi ili majengo yaanze kutumika.
“ Niwatake muongeze kasi ya ujenzi kwa kila hatua mliyofikia ili majengo yaanze kutumika kwani kuchelewesha kwenu mnakwamisha mahitaji ya watumiaji wa majengo haya.” amesema Bi. Maka
Miradi ya Maendeleo ambayo Menejimenti imeweza kutembelea na kukagua ni Ujenzi wa Soko kuu pamoja na ukamilishaji wa miundombinu mbalimbali katika shule ya wasichana shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.