• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

MANISPAA YA SHINYANGA YAZINDUA DAWATI LA USTAWI WA JAMII KUKABILIANA NA UKATILI STANDI YA MABASI MKOA WA SHINYANGA.

Posted on: June 20th, 2025

Katika kuunga mkono juhudi za serikali juu ya kukabiliana na vitendo vya ukatili na kusaidia watoto wanaoishi mitaani, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kwa kushirikiana na shirika la Railway Children Africa, imezindua rasmi Dawati la Ustawi wa Jamii katika Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Shinyanga.


Akizungumza haya leo juni 20, 2025 katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Neema Rwegoshola, amelipongeza shirika hilo kwa juhudi kubwa za kuwajali watoto waishio mitaani huku akisisitiza kuwa kila mwananchi ana wajibu wa kushirikiana na mradi huu ili kusaidia kupunguza ongezeko la watoto hao na kujenga taifa imara la baadaye.


“Tunapaswa kushikamana kama jamii na kuhakikisha watoto hawa wanapata msaada wanaouhitaji. Uwepo wa dawati hili utarahisisha utoaji wa huduma muhimu za ustawi wa jamii na kuwa daraja la matumaini kwa watoto walio katika mazingira magumu hususani eneo hili la standi,” amesema Bi. Rwegoshola.


Kwa upande wake, Meneja wa Mradi kutoka Shirika la Railway Children Africa, Bi. Irene Wampembe, amesema kuwa uanzishwaji wa ofisi hiyo ndani ya standi ni mkakati mahususi wa kufikisha huduma karibu zaidi na wananchi na kuwasaidia watoto wanaoishi mitaani huku akiongeza kuwa lengo ni kuelimisha jamii kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia, kuhamasisha malezi bora, na kufanikisha jitihada za kutokomeza vitendo vya kikatili na unyanyasaji.


Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Ndg. Revocatus Rutunda, amesema halmashauri itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha vitendo vya ukatili vinatokomezwa kabisa ndani ya manispaa ya shinyanga huku akilipongeza Shirika hilo kwa utekelezaji wa mradi huo ndani ya manispaa.


Uzinduzi wa Ofisi hii ndani ya manispaa ya shinyanga ni ushahidi wa dhamira ya dhati ya halmashauri katika kuhakikisha ustawi wa watoto na ustawi wa kijamii kwa ujumla unapata kipaumbele, hasa kwa wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.