- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imejipanga kuendeleza maboma yote yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi ili yaweze kukamilika na kutoa huduma ikiwemo maboma ya vituo vya polisi na zahanati.
Haya yamebainishwa na mkuu wa divisheni ya mipango na uratibu manispaa ya shinyanga Ndg. Mensaria Mrema wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Waheshimiwa Madiwani Katika Mkutano wa Baraza la Madiwani ulioketi kujadili na kupokea taarifa za kata kwa kipindi Cha robo ya pili(Oktoba -Disemba)2024/2025 leo tarehe 6 Februari, 2025.
“kwa upande wa maboma yote ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi kwa mwaka huu wa fedha tunaenda kuyakamilisha kupitia mapato ya ndani ya halmashauri, lakini pia taarifa za maboma hayo tumeshaziwasilisha ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) ili kwa mwaka huu wa fedha yaweze kupewa kipaumbele ili yakamilike na wananchi waweze kupata kuduma kupitia majengo hayo.” Amesema Ndg. Mrema
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amewataka Madiwani kufuatilia uandikishaji wa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato Cha kwanza Kuhakikisha wanaripoti shule hata kama hawana sare za shule kwa kipindi hiki, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kwa wazazi wenye watoto hao.
Naye katibu tawala wa wilaya Shinyanga Ndg. Said Kitinga amewataka Madiwani na wataalamu wa Manispaa ya Shinyanga kutoa elimu ya mikopo ya asilimia kumi ili wananchi waweze kupata mikopo itakayo wawezesha kuondokana na umasikini.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.