- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Ndg. Saidi Kitinga ambae ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Shinyanga leo tarehe 25 Aprili, 2024 ameongoza zoezi la kufanya usafi na kupanda miti katika hospitali ya manispaa ya Shinyanga katika kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea katika zoezi hili Ndg. Kitinga amewashukuru viongozi mbalimbali waliofika katika zoezi hili watumishi pamoja na wananchi wa Manispa ya Shinyanga.
“Niwashukuru viongozi wote , watumishi na Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kuweza kushiriki kwa pamoja katika zoezi hili la usafi katika hospitali yetu pamoja na kupanda miti hakika tumeitendea haki siku ya leo kwa kushikamana na kushirikiana kwa pamoja kama kauli mbiu yetu inavyosema Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “ Tumeshikamana na Tumeimarika kwa Maendeleo ya Taifa Letu.”
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.