- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Utakumbuka kuwa tarehe 11 Agosti, 2024, Manispaa ya Shinyanga tulipokea Mwenge wa Uhuru Ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mapokezi yaliyofanyika katika shule ya Msingi Ibadakuli “A”.
Mwaka huu, tarehe 07 Agosti, 2025, Manispaa ya Shinyanga itapokea tena Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Mapokezi yatafanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nhelegani.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 utakagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Manispaa ya Shinyanga. Hii ni fursa muhimu ya kuonesha mshikamano wetu katika kuunga mkono juhudi za maendeleo.
Ewe Mkazi wa Manispaa ya Shinyanga tunaombwa kushiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mwenge, kuupokea kwenye maeneo utakapopita, na kuhudhuria mkesha wa Mwenge utakaofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.