- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
“ FANYENI KAZI KWA KUZINGATIA SHERIA , KANUNİ NA MIONGOZO YA KIUTUMISHI “ RC MBONI
Na: Shinyanga Mc
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mboni Mhita leo tarehe 24 Julai, 2025 ameongea na watumishi wa halmashauri ya manispaa ya shinyanga katika katika ukumbi wa mikutano wa kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya shinyanga.
Akizunguza na watumishi wa manispaa Mhe. Mhita amempongeza mkurugenzi wa Manispaa ya shinyanga Mwl. Alexius Kagunze kwa utendaji kazi mzuri huku akiwataka watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya utumishi wa umma ili kuweza kuwajibika vizuri katika maeneo yao ya kazi.
“Nikupongeze Mkurugenzi kwa utendaji kazi mzuri katika manispaa yako lakini niwatake watumishi kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kanunia, sheria na taratibu za kiutumishi wa umma ili kusaidia kila mmoja kufanya kazi kwa uwajibikaji na uadilifu katika maeneo yenu ya kazi “. Amesema Mhe. Mhita
Mhe. Mhita amesisitiza pia kwenda kusikiliza na kutatua kero za wananchi kwa wakati, huku akiongezea kuendelea kusimamia vizuri mapato ya ndani kwa kuziba mianya yote inayopoteza mapato, kuendelea kutenga maeneo ya uwekezaji pamoja na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato.
Katika hatua nyengine Mhe. Mhita alipata wasaa wa kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa manispaa na kuwataka mafundi na wasimamizi wa miradi hii kujenga majengo yenye kulingana na thamani ya fedha iliyotolewa na serikali na kumaliza kwa wakati ili wanufaika wa miradi hii waanze kuitumia.
Miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Mhe. Mhita ni ujenzi wa shule mpya ya sekondari Ishigwandama kata ya Kizumbi, ujenzi wa zahanati ya mwamagunguli Kata ya kolandoto, Ujenzi wa madarasa 2 shule ya msingi Kambarage kata ya Kambarage, Ujenzi wa ofisi za machinga kata ya lubaga, ubanuzi wa mtandao wa maji pamoja na Ujenzi wa barabara ya kenyata hadi karena .
Ziara hii ya Mhe. Mhita ni muendelezo wa ziara zake za kikazi katika halmashauri zote sita zinazojumuisha mkoa wa shinyanga kwa lengo la kutembelea , kukagua miradi ya maendeleo pamoja na kuongea na watumishi wa halmashauri hizo.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.