• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Complaint |
Shinyanga Municipal Council
Shinyanga Municipal Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Shinyanga Municipal Council

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Core values
    • Strategies
  • Administration
    • Administration Boundary
    • Organization Structure
    • Departments
      • Human resource
      • Secondary Education
      • Primary School
      • Finance
      • Works
      • Agriculture and Cooperative
      • Livestock and Fisheries
      • Water
      • Community Development, Social Welfare and Youth
      • Planning, Monitoring and Statistics
      • Hearth
      • Cleaning and Environment
      • Land and Natural Resources
    • Units
      • Information, Communication, Technology and Public Relations
      • Legal
      • Internal Auditor
      • Election
      • Procurement Management
      • Beekeeping and Forest
  • Investment Opportunities
    • Industrialization
    • Farming Opportunity
    • Livestock Keeping
    • Fish breeding
    • Education Opportunity
    • Health Opportunity
  • Our Service
    • Health services
    • Education services
    • Water Services
    • Agriculture Services
    • Livestock Services
    • Fish breeding
    • Huduma za Watumishi
    • Loans Services
    • Service to rent business rooms
    • Sewage Sanitation Services
    • Business Services
      • Business License
      • Business education
      • Industrial auditing
      • Market Managent
      • Prepalation of Good Environment for Investment
  • Councilors
    • List of councilors
    • Committees
      • Finance and Administration Committee
      • Economics, Health and Education Committee
      • Infrastructure Committee
      • Control Aids Committee
      • Ethics Committee
    • Committees Timetable
  • Projects
    • Approved projects
    • On Progress Projects
    • Complete Projects
  • Publications
    • Municipal Bylaws
    • Customer service agreement
    • Strategic plan
    • Reports
    • Application Forms
    • Guidelines
    • Newsletter
  • Media Center
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • Video
    • Training

DC SHINYANGA AONYA SIASA ZA MAJITAKA MWAMAGUNGULI

Posted on: June 21st, 2017

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewaonya wananchi wa kijiji cha Mwangunguli kata ya Kolandoto katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuacha tabia ya kuwasikiliza viongozi wa siasa ambao wanahujumu juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo. Mheshimiwa Josephine Matiro ameyazungumza hayo katika kijiji hicho alipoenda kuwasikiliza maoni ya wananchi ikiwa ni mojawapo ya kituo maalumu kati ya vituo mbalimbali  vilivyotengwa kusikiliza maoni ya wananchi katika juma zima la Utumishi wa Umma.

Mmoja wa wananchi Shija Luhende akieleza mbele ya mkuu wilaya kuwa maji hayafai- (Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)

Baada ya kufika katika kijiji hicho akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa, walizungumza na wananchi wa eneo hilo ambapo hoja ya mgogoro wa mradi wa maji ya kisima kirefu katika kijiji hicho ilisikilizwa.Ilielezwa kuwa mradi huo wa maji ambao ujenzi wake ulikamilika mwaka 2014 kwa gharama ya shilingi 294.6 ulikuwa haujatumika kuhudumia wananchi kutokana na propaganda zilizokuwa zikienenezwa na viongozi wa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi kata wakidai kuwa maji ya kisima hicho yana chumvi na hata yakitumika kupikia chakula yanakibadilisha na kuwa na rangi ya njano.

Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akinywa maji yaliyoaminika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu-(Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)

Kufuatia utata huo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa Geoffrey Ramadhan Mwangulumbi na baadhi ya wananchi waliamua kunywa maji na kuagiza chakula kipikwe kwa kutumia maji hayo ili wathibitishe kama maji hayo yana chumvi pia kama yanabadilisha chakula kuwa cha njano. Mara baada ya kunywa maji hayo, mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na wananchi wote walithibitisha kuwa maji hayo hayana chumvi na yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

Na mara baada ya chakula ‘wali’ kupikwa katika nyumba iliyokuwa jirani na eneo la mkutano, kililetwa mbele ya mkutano na kuwaonyesha wananchi rangi ya chakula inayoonekana baada ya kupikwa kwa kutumia maji ambayo yalitangazwa na viongozi wao kuwa yanabadilisha rangi ya chakula. Chakula kilicholetwa kilikuwa na rangi nyeupe kama ilivyo kawaida ya rangi ya chakula hicho, hali ambayo ilisababisha minong’ono miongoni mwa wananchi na baadhi ya viongozi wao wa kisiasa kuanza kuondoka wakiwa na aibu tele.

Baada ya kunywa maji na kuona chakula hakijabadilika rangi, mkuu wa Wilaya alisema kuwa amegundua kuwa viongozi wa kijiji hicho ambao ni wanasiasa wamewasababishia wananchi wao shida wakiwemo akina mama na watoto kutembea umbali mrefu wakitafuta maji na kuacha maji yaliyo karibu na makazi yao. Mara baada ya kutatua mgogoro huo, mkuu wa Wilaya aliukabidhi mradi huo kwa wananchi wa kijiji wakishirikiana na wataalam  wa Manispaa.

Mkurugenzi wa Manispaa akionesha chombo kitupu mara baada ya kunywa maji ambayo yaliyokuwa yakipotoshwa na vingozi wa siasa kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.(Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)

Mwananchi wa Kijiji cha Mwamagunguli akinywa maji ya maradi uliokuwa na mgogoro kuwa maji yake yana chumvi na yanabadilisha rangi ya chakula.(Picha kwa hisani ya Marco Maduhu na Malunde Blog)


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MADEREVA April 14, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA April 27, 2023
  • MAADHIMISHO YA WIKI YA UNYONYESHAJI WA MAZIWA DUNIANI August 04, 2023
  • TAARIFA KWA UMMA MAONESHO YA NANENANE 2023 July 31, 2023
  • View

Latest News

  • RC MHITA AKABIDHIWA RASMI OFISI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

    July 01, 2025
  • BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.

    June 25, 2025
  • MANISPAA YA SHINYANGA YASAINI MIKATABA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA MIJI TANZANIA.

    June 25, 2025
  • SALAMU ZA PONGEZI

    June 24, 2025
  • View

Video

MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA 2024
More Videos

Quick Links

  • Tangazo la nafasi ya kazi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
  • Urban Sanitation and Hygiene | Mazingira Safi Maisha Bora
  • Varios Report
  • Council bylaws

Related Links

  • President's Office Regional Administration and Local Government
  • President's Office Public Service Management
  • Ministry of Education,Science and Technology
  • The National Examinations Council of Tanzania
  • Shinyanga Region
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Contact Us

    Tanesco S, Mwanza Road

    Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga

    Telephone: +255-28-2763213

    Mobile: 0759 023 788

    Email: md@shinyangamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sitemap
    • Sera ya faragha
    • Kanusho

Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.