- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julias S. Mtatiro ametoa siku Saba kwa maafisa tarafa, walimu wakuu wa Shule, Waratibu Elimu kata pamoja watendaji wa Kata kutoka halmashauri ya Manispaa ya shinyanga kuwasaka jumla ya watoto 26 waliosalia kujiunga na kidato cha kwanza licha ya kufaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2025.
Wakili Mtatiro ametoa maelekezo haya leo Februari 18, 2025 kwenye kikao kazi cha udahili wa wanafunzi ambao hawajaripoti na kujiunga na masomo ya kidato cha kwanza, kikao kilichofanyika Katika ukumbi wa mikutano chuo Cha Ualimu Shinyanga SHYCOM Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
“Niwapongeze sana kwa juhudi mlizochukua kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti shule, lakini hawa wanafunzi 26 natoa muda wa siku saba tu kuwasaka walipo, ikiwa ni Pamoja na kuwachukulia hatua za dhati kwa wazazi na walezi wa Watoto hao ili waripoti shule mara moja, kuanzia leo mpaka tarehe 28 wawe wameripoti shule Watoto hao, nje na hapo nitaunda kikosi kazi mahili kitakachokwenda kuwarudisha Watoto hao, haiwezekani Serikali itumie nguvu nyingi kujenga miundombinu mizuri, bora na rafiki kwa ajili ya Watoto hao harafu mzazi, au mlezi akatishe ndoto zao, mimi kama Mkuu wa wilaya nitahakikisha kwa nguvu zangu zote swala hili nalishughulikia ipasavyo”. Amesema Wakili Mtatiro
Kwa upande mwingine Wakili Mtatiro amewataka walimu wakuu kuwasimamia walimu Katika swala la ufundishaji ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi, huku akiutaka uongozi wa manispaa ya shinyanga kuandaa siku ya kuwapongeza walimu na shule za Sekondari zilizofanya vizuri Katika mitihani ya kidato Cha nne.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa Mwaka wa Masomo 2025 Jumla ya wanafunzi 4,274 wavulana wakiwa ni 1,867 na Wasichana wakiwa 2,407. Walichaguliwa kijiunga na masomo ya kidato cha kwanza.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.