- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Wakili Julius Mtatiro ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga leo tarehe 24 Februari, 2025 ameongoza zoezi la upandaji miti katika wiki ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani ambapo pamoja na shughuli nyingi walizofanya Jumuiya ya Maridhiano ya Mkoa wamepanda miti katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na eneo la Foresti lililopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza katika zoezi hili la upandaji miti Wakili Mtatiro ameipongeza Jumuiya ya Maridhiano na Amani ya Mkao kwa kuamua kupanda miti ikiwa ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa ya kijani ili kukabiriana na mabadiliko ya tabianchi.
“Niwapongeze Jumuiya ya Maridhiano na Amani ya Mkoa kwa kuazimisha wiki ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani kwa kupanda Miti ikiwa ni kumuunga mkono Rais Wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuzidi kuifanya Tanzania yetu iwe ya Kijani na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.” Amesema Wakili Mtatiro
Kwa upande wake mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani ya Mkoa wa Shinyanga Sheikh Massoud Ramadhani Mloye amesema wao kama kamati ya maridhiano na amani ya mkoa wa shinyanga hawapo tayari kuona amani , mila na desturi zinapotea hivyo nijukumu lao kushirikiana na serikali ili kutunza amani , mila na desturi za nchi yetu.
Kilele cha Maadhimisho ya Jumuiya ya Maridhiano na Amani kitaifa yatafanyika Mkoa wa Arusha ambapo Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani atakuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo tarehe 26 Februari 2025.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.