- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
BOTI MPYA YA UOKOAJI ZIWA VICTORIA YAWASILI MANISPAA YA SHINYANGA.
Na: Shinyanga MC
Wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wamejitokeza kwa wingi kushuhudia usafirishaji wa boti maalum ya uokoaji (Ambulance Boat) ikisafirishwa kutoka Mtwara kuelekea Mkoa wa Mwanza kupitia mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kutoa huduma katika Ziwa Victoria.
Boti hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha huduma za dharura, hasa kwa wananchi wanaofanya shughuli za uvuvi na usafiri wa majini katika maeneo ya mwambao wa Ziwa Victoria.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo, huku wakieleza kuwa ujio wa boti hiyo ni ushahidi wa wazi wa namna Serikali inavyowajali wananchi wake na kuendelea kuboresha huduma muhimu za kijamii hususan katika sekta ya afya na usalama majini
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.