- Home
- About Us
- Administration
- Investment Opportunities
- Our Service
- Councilors
- Projects
- Publications
- Media Center
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, amejiandikisha kwenye daftari la wakazi kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Askofu Sangu amejiandikisha ya leo Novemba 20,2024 kwenye kituo cha Shule ya Msingi Bugoyi (A) mtaa wa Mbuyuni kata ya Ndemebezi Manispaa ya Shinyanga, ikiwa ni siku ya mwisho .
Akizungumza mara baada ya kujiandikisha, Askofu Sangu amewasisitiza wananchi kujiandaa kikamilifu kutumia haki yao ya Kikatiba,kuwachagua viongozi wanaowataka kwa kujitokeza kwa wingi siku ya Uchaguzi, kuhu akitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani
Viogozi watakaochaguliwa kupitia uchaguzi huo wa Serikali za mitaa ni pamoja na Wenyeviti wa Mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe wao.
Tanesco S, Mwanza Road
Postal Address: P.O.Box 28 Shinyanga
Telephone: +255-28-2763213
Mobile: 0759 023 788
Email: md@shinyangamc.go.tz
Copyright ©2018 Shinyanga Municipal Council . All rights reserved.