- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WATUMISHI WA UMMA MANISPAA YA SHINYANGA NA TAASISI ZAKE WAPATA MAFUNZO
Na. Shinyanga Mc
Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imeendelea kutoa mafunzo ya kutumia mfumo mpya utakaotumika kupima utendaji kazi kwa watumishi wa umma pamoja na taasisi zake.
Mafunzo haya yaliyofunguliwa tarehe 20 Novemba, 2023 na Mwl. Dafroza Ndalichako ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo yanahusisha Taasisi na Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga
Serikali imekusudia kuondokana kabisa na mfumo wa awali uliokuwa unatumika kupima utendaji kazi kwa watumishi (OPRAS) na kuanza kutumia PEPMIS na PIPMIS sambamba na mfumo mpya wa kufanya tathimini ya Rasilimali Watu ofisini HR - ASSESMENT, ambapo utasaidia kutambua idadi halisi ya watumishi katika ofisi.
Mafunzo haya yanaendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu Mkoa wa Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga