- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WATENDA WA KATA, MITAA NA VIJIJI WATAKIWA KUSIMAMIA UKUSANYAJI WA MAPATO YA NDANI.
Na. Shinyanga Mc
Watendaji wa kata, Mitaa na vijiji watakiwa kuwa mstari wa mbele katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuendelea kuleta maendeleo katika kata zao na Manispaa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze katika kikao kazi cha watendaji wa kata, mitaa ,vijiji pamoja na Maafisa afya kilichofanyika leo tarehe 4 Julai, 2024 katika ukumbi wa lewis kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga.
“Kazi moja wapo ya utendaji wa kata,vijiji na mitaa ni kusimamia na kulinda ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri ili yasipotee” amesema Mwl. Kagunze
Aidha , Mwl. Kagunze amewata kwende kusimamia mapato hayo ya ndani ikiwemo kukusanya ushuru wa huduma, kodi ya mapango, vibali vya ujenzi pamoja na kuwahamasisha wafanyabiashara wote wanaofanya biashara sehemu ambazo sio rasmi na badala yake kwenda kufanyia biashara sehemu rasmi zinazotambulika na serikali,
Pamoja na mambo mengine Mwl. Kagunze amewapongeza kwa usimamizi mzuri wa mazingira mpaka kufikia hatua ya ushindi wa kwanza kitaifa kati ya halmashauri 184 na kuwataka kuendela kusimamia usafi wa mazingira kwa kushirikiana na Maafisa afya ili kuendela kuwa wasafi kitaifa.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga