- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WANAFUNZI KUTOKA SHULE 20 ZA MANISPAA YA SHINYANGA WAKUTANA KUBADILISHANA UJUZI ILI KUBORESHA TAALUMA
Na: Shinyanga MC
Katika juhudi za kuinua viwango vya taaluma kwa wanafunzi wa sekondari, Idara ya Elimu Sekondari Manispaa ya Shinyanga imeandaa hafla maalum iliyowakutanisha wanafunzi kutoka shule 20 za Sekondari zilizopo ndani ya Manispaa hiyo. Hafla hiyo imefanyika leo, Mei 17, 2024, katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Wasichana Shinyanga.
Tukio hilo limewaleta pamoja wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne pamoja na walimu wao kwa lengo la: Kubadilishana maarifa ya kitaaluma, Kukuza vipaji vya wanafunzi, Kujenga mahusiano chanya miongoni mwao, Kuweka mikakati ya pamoja ya kuinua ufaulu katika Manispaa ya Shinyanga.
Akifungua rasmi hafla hii mgeni rasmi ambaye ni Mthibiti Ubora wa Elimu wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Edith Mwijage, amewahimiza wanafunzi kuwa na shauku ya kujifunza kila siku, kutafuta maarifa mapya, na kujiepusha na makundi yasiyofaa ili kufikia ndoto zao. Aidha, huku akiwahimiza walimu kuandaa matukio kama haya mara kwa mara kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na maarifa.
Naye Afisa Elimu Taaluma Sekondari wa Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Richard Makoye, amesema kuwa tukio hilo limeandaliwa kwa makusudi ili kuwapa wanafunzi jukwaa la kuonyesha uwezo wao wa kitaaluma, kujifunza kwa wenzao, na kuhamasishwa zaidi katika masomo.
Kwa upande wake Mwl. Greyson George, akiwasilisha mada amesisitiza umuhimu wa mwanafunzi kuwa na ratiba ya masomo, kuepuka matumizi mabaya ya muda, na kuwa na bidii ya masomo, pamoja na kujiamini na kushirikiana na walimu ni nguzo muhimu za mafanikio.
Ikumbukwe kuwa, Manispaa ya Shinyanga kwa mwaka wa Elimu 2024 iliongoza kwa ufaulu kwa asilimia 97% kati ya Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga, mafanikio haya yakiakisi jitihada endelevu za Idara ya Elimu Sekondari kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga inaendelea kuimarisha elimu kwa kushikilia kauli mbiu yake isemayo :”SHINYANGA MUNICIPAL LET’S PUSH TOGETHER: I MUST, I WILL, I CAN.”
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga