- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mhe. Kanali Evans Mtambi mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane kanda ya ziwa mashariki ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mara amewataka wakulima kuachana na kilimo cha kubahatisha na badala yake kutumia njia sahihi za kilimo bora ili kujipatia mazao bora na yenye thamani .
Mhe. Mtambi ameyasema hayo leo Agosti 8,2024 wakati akizungumza kwenye kilele cha sikukuu ya wakulima Nane Nane kanda ya Ziwa mashariki, maonyesho yaliyowakutanisha wakulima, wataalam wa kilimo na ufugaji kutoka Mikoa mitatu Shinyanga Mara pamoja na Simiyu yaliyofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Baridi Mkoani Simiyu na kuwataka wakulima kuachana na kilimo cha kubahatisha.
“ kilimo cha kubahatisha kimepitwa na wakati hebu tubadilike wakulima, Shughuli za kilimo na ufugaji zikiendeshwa vizuri zinatija katika sekta ya kilimo, mafunzo haya na semina hizi tulizopata tangu tarehe 1 kutoka kwa wataalamu wa kilimo na ufugaji hebu twendeni tukazitumie kwa usahihi.” amesema Mhe
Mtambi
Pamoja na mambo mengine Mhe. Mtambi amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili kuchagua viongozi bora kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa uwepo wa maonesho haya kwa kanda ya Ziwa Mashariki ni fursa kubwa sana kwa wananchi wa Mikoa hii mitatu ya Shinyanga , Mara na Simiyu kwani imekutanisha wataalam wa Serikali, Taasisi na Sekta binafsi.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga