- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
WAANDISHI WASAIDIZI NA WAENDESHAJI WA VIFAA VYA BAYOMETRIKI WAPATIWA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU II.
Na. Jesca Kipingu
Waandishi Wasaidizi na Waendeshaji wa Vifaa vya Bayometriki wapatiwa mafunzo ya uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura Awamu ya pili leo Marchi 28, 2025 katika ukumbi wa shule ya Maalum ya Buhangija iliopo Manispaa ya Shinyanga.
Akifungua mafunzo haya Afisa mwandikishaji Jimbo la shinyanga Mjini Mwl. Alexius Kagunze amewataka waandishi kuwa makini katika mafunzo haya kwakuwa baada ya mafunzo watakwenda kufanya kwa vitendo hivyo ni bora umakini uwepo ili kufanya kazi kwa waledi zaidi.
Awali waandishi Wasaidizi na Waendeshaji vifaa vya bayometriki walikula viapo vya aina mbili ikiwemo kiapo cha tamko la kijitoa katika vyama vya siasa na kiapo cha kutunza siri ambapo vyote hivyo viliongozwa na afisa Mwandikishaji Jimbo la shinyanga Mjini.
Pamoja na mambo mengine Mwl. Kagunze ametoa wito kwa waandishi kwenda kutunza vifaa vyote watakavyokabidhiwa na kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Afisa mwandikishaji na wasaidizi wake ili kuweza kufanya kazi kwa weledi.
Daftari la kudumu la Wapiga kura awamu ya pili litaanza rasmi tarehe 1-7 Mei 2025 ambapo jumla la vituo 25 vya kujiandikishia vitatumika katika Kata zote 17 za manispaa ya Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga