- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Vyama vya Siasa wilayani Shinyanga Vimeaswa Kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi ili kuepusha uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024.
Haya yamezungumzwa leo Oktoba 22,2024 Na Ndg. Frank Shija Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa Tanzania aliye fika wilayani Shinyanga kwa lengo la kuwakumbusha Majukumu, wajibu na haki kwa vyama vya siasa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
“Kutokana na Sheria ya vyama vya siasa Sura ya 258 chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kinawajibu wa kuheshimu Sheria,kanuni za uchaguzi,kulaani,kuepuka na kuchukua hatua zinazofaa ili kuzuia au kuepusha vitendo vya vurugu,lugha ya matusi,pamoja na uvunjifu wa amani”. amesema
Ndg. Shija.
Kwa upande wake Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mwl. Alexius Kagunze amewataka viongozi hao wa vyama vya siasa kuwahamasisha wanachama wao, na wananchi kwa ujumla kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, ili kupata viongozi bora watakao waletea maendeleo.
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika Novemba 27, 2024.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga