- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS) (FFARS) kupitia mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na mradi wa Tuimairishe Afya-HPSS (Health Promotion and System Strengthening) yameanza leo katika hoteli ya Vigmark mjini Shinyanga.
Zaidi ya washiriki 60 katika makundi ya waratibu elimu kata katika kata zote za Halmashauri ya Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, mkuu wa kituo cha afya na mhasibu wa kila hospitali ya wilaya wamepatiwa mafunzo ya Mfumo wa FFARS katika vituo vya kutolea huduma zikiwemo zahanati, vituo vya afya, hospitali na shule za msingi na sekondari.
Mojawapo ya kundi la washiriki wa semina wakiwa kwenye mazoezi ya vitendo ya ujazaji wa daftari la fedha katika sekta ya afya na elimu
Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha washiriki hao ili waweze kuufahamu mfumo na kuweza kwenda kutoa mafunzo ya utumiaji wa mfumo wa FFARS kwa watoa huduma waliopo katika ngazi za shule za msingi na sekondari, na vituo vya afya wakiwemo kila mkuu wa kituo cha afya, mhasibu wa kila shule ya msingi na sekondari.
Mafunzo ya leo ni matokeo ya mafunzo yaliyofanyika tarehe 5 hadi 6 Juni 2017 ambapo wahasibu zaidi ya 130 kutoka Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji kwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kati walipatiwa mafunzo ya Mfumo wa FFARS ambao kwa leo wamekuwa wawezeshaji kwa washiriki zaidi ya 60 waliohudhuria mafunzo. Wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka PS3, TAMISEMI, Wizara ya afya, HPSS (Health Promotion and System Strengthening) na Wizara ya Elimu wameshiriki katika kutoa mafunzo kwa kuhakikisha mafunzo yanaendeshwa kwa ufanisi wenye matokeo chanya.
Wakati akifungua mafunzo, mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3, Dr. Suma Kaare, alisema mfumo wa kutumia njia za kielektroniki (kompyuta) katika kuingiza taarifa za kifedha za vituo vya kutolea huduma utasaidia kurahisisha kazi na tayari serikali imeukubali na utaanza kutumika kuanzia mwezi Julai, 2017 katika halmashauri mbalimbali.
Dr. Suma Kaare, Mkuu wa Idara ya Ufuatiliaji, Tathmini na Tafiti Tendaji kutoka PS3.Kulia ni Bi.Catherine Oyoga Mhasibu katika Mifumo ya Fedha TAMISEMI
Baada ya mafunzo haya, wahitimu wataenda kutoa mafunzo katika vituo vya kazi vinavyotoa huduma kuanzia tarehe 19 hadi 30 Juni 2017. Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ina jumla ya vituo vya Serikali 76 vinavyotoa huduma katika sekta ya Elimu na Afya ambavyo vitaanza kutumia mfumo wa FFARS kutoa taarifa za fedha. Kuna Shule za Msingi 48, shule za sekondari 17, vituo vya afya 1, zahanati 9 na Hospitali 01 yenye hadhi ya 'Council Designed Hospital' iliyopo Kolandoto.
Bonyeza hapa kupakuwa mada zilizofundishwa kwa washiriki wa semina
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga