- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
VIONGOZI WA HALMASHAURI YA JIJI LA DAR-ES-SALAAM WAWASILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA.
Na. SHINYANGA MC
Kamati ya Fedha na Utawala, Wakuu wa Divisheni na Vitengo Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam wamefika katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiongozwa na Mhe. Omar Kumbilamoto Mstahiki Meya Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam kwa lengo la kujifunza namna ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na Upendezeshaji Mji.
Wakiwa Manispaa ya Shinyanga Viongozi hao waliweza kupata muda wa kujifunza mambo mbalimbali kwa njia ya mawasilisho na vitendo namna ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha za Mapato, Wahisani na Serikali kuu.
Akitoa salama za Halmashauri ya Jiji la Dar-es-salaam Mhe. Omar Kumbilamoto wamekuja Shinyanga kwa lengo la kujifunza namna ya utekelezaji wa miradi, kuimarisha uhusiano na kufahamiana.
‘’Tumekuja hapa kwa lengo la kujifunza namna bora ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kubadilishana uzoefu wa mambo mbalimali’’ alisema Mhe. Kumbilamoto
Pamoja na mambo mengine Viongozi hao waliweza kufanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya miradi ya maendeleo kama Soko kuu la Ibinzamata,Soko kuu,Ngokolo Mitumbani, Machinjio ya Kisasa NdembezKituo cha afya kamabarage kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi, wagonjwa wa nje [OPD], Jengo la mionzi na shule ya msingi Jomu madarasa matano.
Pia walipata wasaa wa kutembelea maeneo yaliyopendezeshwa [Beutification kama maporomoko ya maji maeneo ya mto kidalu/relini, Round About ya police, karogo, eneo la mapumziko NBC na Sanamu yenye kuonesha asili ya watu wa Mkoa wa Shinyanga na shughuli zinazofanya na wakazi wa mkoa huu maeneo ya relini/tandale.
Aidha, kwa upande wa Manispaa ya Shinyanga timu iliongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Elias Masumbuuko pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo na Watendaji wa kata iliwashukuru kwa kuichagua Manispaa ya Shinyanga kama sehemu yao ya kujifunzia na kwamba uongozi wa Manispaa pamoja na mambo mengine umewakaribisha wakati mwengine na kuwaalika Halmashauri nyengine kuja kujifunza mambo mengine mazuri.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga