- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Katika Kuhakikisha jamii inaondokana na umasikini na kujikwamua kiuchumi Manispaa ya Shinyanga imetoa mafunzo kwa jumla ya vikundi (19) vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, vikundi vilivyokidhi kupata mkopo wa asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani mikopo isiyo na riba.
Akizungumza leo Machi, 22,2025 katika mafunzo haya Afisa maendeleo ya jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga Bi. Nyanjula Kiyenze amesema jumla ya Tsh. Milion 225,879,500/= zimetengwa kwa ajili ya vikundi hivyo ambapo Kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 2024 inatutaka kabla ya vikundi vilivyokidhi kupata mkopo havijapokea ni lazima vipate mafunzo ili kuongeza uelewa juu ya mkopo huo.
“jumla ya Tsh milioni 225,879,500/= ambapo vikundi vya wanawake ni Tsh 127,927,500/= vikundi vya vijana Milioni 123,952,000/= na Mtu mwenye ulemavu ni Tsh 4,000,000/= zimetolewa na halmashauri mikopo ya asilimia kumi isiyokuwa na riba ili vikundi hivi viweze kujikwamua kiuchumi”. Amesema Bi. Nyanjula.
Awali akifungua mafunzo haya Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko amevisisitiza vikundi hivyo kuwa na nidhamu ya Fedha, kuwa waaminifu Katika kurejesha mikopo hiyo ili iweze kuwanufaisha wananchi wengine.
“Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inafanya kila liwezekanalo Kuhakikisha makundi haya yanajikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini, fedha hizi ni mapato ya ndani ambayo ni Kodi za wananchi, sasa niombe kuwa na nidhamu ya fedha hizi, kuweni waaminifu Katika kurejeshe ili vikundi vingine navyo vipate kama ninyi mlivyopata. Amesema”. Mhe Masumbuko
Katika vikundi hivyo jumla ya mada (5) zimefundishwa Usimamizi wa vikundi, Utatuzi wa migogoro, Usimamizi wa biashara, Utunzaji wa kumbukumbu pamoja na Msaada wa kisheria (MSLAC) zimefundishwa kwa vikundi 19 kutoka kata 9 kati ya Kata 17 za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga zilizokidhi kupata mkopo huo.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga