- Mwanzo
- Kuhusu sisi
- Utawala
- Fursa za Uwekezaji
- Huduma Zetu
- Madiwani
- Miradi
- Machapisho
- Kituo cha Habari
Na George Mganga, SHY MC
UJUMBE wa RS Mkoa wa Kilimanjaro ukiongozwa na Katibu Tawala Msaidizi wa Sehemu ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mkoa wa Kilimanjaro Bi. Halima F. Hassan, leo umetembelea Kituo cha Urasimishaji Uwekezaji na Uendelezaji Biashara kilichopo Mnara wa Vodacom katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya Uwekezaji.
Katika ziara hiyo, Bi. Halima alipata nafasi ya kushuhudia Ofisi za kituo hicho ambacho kimejengwa kwa Fedha za Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA), kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia mapato yake ya ndani.
Mbali na kushuhudia, Bi. Halima alipata nafasi ya kujifunza namna MKURABITA inavyowezesha Halmashauri juu ya upatikanaji wa Vituo vya Uwekezaji, na namna ya kuwaendeleza wananchi kiuchumi ili kufikia malengo yao kupitia Manispaa ya Shinyanga.
Aidha, huduma zinatolewa katika kituo hicho ni huduma ya Leseni, Kurasimisha Biashara Ndogo na za Kati, Kuratibu masuala mazima ya Uwekezaji na kutoa Elimu kwa wafanyabishara juu ya elimu ya biashara.
Katika ziara hiyo Bi. Halima aliambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Ndg. Rashid K. Gembe, Afisa Biashara Mkoa wa Kilimajaro Ndg James Bwanali na Charles Kagembe ambaye ni Mhandisi wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa upande wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga iliwakilishwa na Bi. Milembe G. Dabana ambaye ni Afisa Biashara Divisheni ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, Bi. Paschazia Makongolo kutoka Ofisi ya Mchumi, halikadhalika Mhandisi Maligisa Dotto Kaimu Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Sektretarieti ya Mkoa wa Shinyanga, pamoja na Rose Tungu ambaye ni Afisa Biashara, Sekreterieti ya Mkoa wa Shinyanga.
Tanesco S, Mwanza Road
Anwani ya Posta: P.O.Box 28 Shinyanga
Simu: +255-28-2763213
Simu ya Mkononi: 0759 023 788
Baruapepe: md@shinyangamc.go.tz
Haki zote zimehifadhiwa@2018.Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga